Chelsea yainyuka Middlesbrough tatu bila
Chelsea inayo nafasi moja tu kufikia
kileleni mwa ligi baada ya kuichabanga timu ya Middlesbrough kwa bao
tatu kiduarisho katika uwanja wa Stamford Bridge.
Antonio Conte
aliwabugiza Middlesbrough kwa magoli baada ya kupokea pasi iliyotakata
kutoka kwa Diego Costa, Marcos Alonso na Nemanja Matic, na huenda
Chelsea watatawazwa kuwa vijogoo wa ligi kuu ya England endapo
watafanikiwa kuvuka kihunzi katika uwanja wa West Bromwhichalbion siku
ya ijumaa.
Chelsea walicheza kwa kujiamini mithili ya mabingwa,
hata kama hawatashinda mwishoni mwa wiki dhidi West Brom , Chelesea
inakabiliwa na mechi za nyumbani watford na Sunderland kujishindia taji
la pili katika misimu mitatu.
Chelsea walishajitengenezea
mazingira ya ushindi kabla hata Diego Costa hajageuza mchezo na yeye
kuwa nyota wa mchezo baada ya kugongewa pasi murua na Cesc Fabregas
katika dakika ya ishirini na tatu ya mchezo.
Mchezo ulinoga zaidi
wakati Marcos Alonso alipopachika bao lingine kwa kuunyakua mpira
miguuni mwa kipa wa timu ya Middlesbrough Brad Guzan dakika kumi na moja
kabla ya kipyenga cha mapumziko .
Naye Cesc Fabregas iliingizia Chelesea goli la tatu na la lala salama.
Marcos Alonso akitumia vizuri mpira wauliopigwa na Cesar Azpilicueta na kufunga bao la pili dhidi yaMiddlesbrough katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Stamford Bridge jijini London usiku wa kuamkia leo.
Alonso akipongezwa na wenzake, Cesc Fabregas (kulia), na Diego Costa baada ya kuifungia timu yake bao la pili.
Nemanja Matic akipiga mpira uliozaa bao la tatu.
Benchi la ufundi la Chelsea likishangilia ushindi |
Costa akijaribu kumtoka Fabio Middlesbrough |
Matic akishangilia bao alilofunga dhidi ya Middlesbrough usiku wa kamkia leo.
No comments