BENKI YA KILIMO YAOMBWA KUTOA MIKOPO ARUSHA
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Richard Kwitega (kushoto), akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Francis
Assenga (kulia), wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa
za uwekezaji mkoani Arusha.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Richard Kwitega (katikati), akizungumza na ugeni kutoka TADB,
wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji
mkoani Arusha. Ugeni uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Richard Kwitega akihimiza jambo wakati alipokuwa akizungumza
na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia
fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis Assenga (kushoto) ,
akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega
(hayupo pichani), wakati walipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia fursa
za uwekezaji mkoani Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara
wa TADB, Augustino Chacha.
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara
wa TADB, Augustino Chacha (kulia), akizungumzia fursa za mikopo
inayotolewa na Benki wakati akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Richard Kwitega (hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis
Assenga.
Meneja wa Uendelezaji wa Biashara
wa TADB, Geofrey Mtawa (kulia) akitoa takwimu za mahitaji ya mikopo
ya mkoa wa Arusha. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Uendelezaji wa
Biashara wa TADB, George Nyamrunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Richard Kwitega (kushoto) akimkabidhi muhtasari wa maeneo ya
uwekezaji Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
(TADB), Francis Assenga.
………………………………..
Na Mwandishi wetu,
Wito umetolewa kwa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), kuchangamkia fursa za uwekezaji
katika serkta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo wakulima
wanaojishughulisha katika sekta hizo mkoani Arusha ili kuchagiza sekta
ya kilimo mkoani humo.
Wito huo umetolewa na Katibu
Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega wakati akizungumza na
ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia
fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Bw. Kwitega amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo na ufugaji.
Akizungumza wakati wa mazungumzo
hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Francis Assenga
alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa
uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta
mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na
mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi
zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.
Assenga mkoa wa Arusha
utaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa
wakulima na wafugaji wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotolewa
na TADB.
No comments