102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’
Mwandishi wetu, Mwanza
Kituo cha Redio cha 102.5 Lake FM kimezindua kampeni ya kufanya
usafi kwa jijini la Mwanza ijulikanayo kwa jina la Ng’arisha Nzengo,
Uchafu Nuksi yenye lengo la kuufanya mji huo kuwa msafi zaidi.
Mkurugenzi wa kituo hicho Doreen Estazia Noni amesema kuwa
wameamua kuanzisha kampeni hiyo ya usafi ili kuupendezesha zaidi mji huo ambao
ni minongoni mwa miji mikubwa hapa nchini.
Doreen amesema kuwa moja kati ya vipaumbele vya kampuni ya Lake
Fm nikuhakikisha inatoa mianya ya kuiwezesha jamii kufikia kusudi la maendeleo
binafsi na jamii nzima kwa ujumla.
“Neno ni la kabila ya Wasukuma lenye maana ya nyumbani, tumeamua
kutumia neon hili ili kufikisha ujumbe haraka kwa wakazi wa jiji la Mwanza,
kampeni hii ni endelevu kituo chetu cha redio kitaendelea
kuhamasisha mpaka kufikia lengo letu,”
“Kituo chetu cha redio kimeamua kupanua wigo wake kwa
kujihusisha katika masuala mbalimabli ya kijamii na kutatua changamoto
mbalimbali na kuleta mtazamo chanya na si kuhabarisha na kuburudisha
tu, naomba ushirikiano mkubwa kwa wadau, serikali
na watu binafsi katika kufanikisha kampeni hii,” alisema Doreen.
Mbali ya 102.5 Lake FM, kampeni hiyo pia imewashirikisha wadau wengine
kama Baamedas tv, Genic Studios , viongozi wa Jumuiya ya biashara ndogondogo,
minada na masoko , mwenyekiti Justin Sagala, mwenyekiti wa Afya Minadani,
Gosbert Lucas, katibu wa afya, Mariam Magembe, kiongozi wa wa madereva wa
daladala Dede Petro, serikali na Asasi binafsi.
Mkuu wa maudhui na vipindi wa redio
hiyo, Yusuph Magupa ambaye pia ni mwenyekiti wa kampeni hiyo amesema
kuwa afya ni ghali na wakazi wa Mwanza wanapaswa kuishi katika
mazingira salama ili kulinda afya yako.
Kupitia uzinduzi wa kampeni hii iliyozinduliwa rasmi siku ya
jumatatu ya Mei Mosi, katika kipindi cha asubuhi cha Kokoliko, Magupa
amebainisha mpango mkakati wa kampeni hiyo kuwa nikuhakikisha elimu ya usafi
kwa afya bora inaeleweka na kuzingatiwa katika jamii.
Katibu wa kampeni hii, Iman Hezroni ambaye ni pia ni
mtangazaji wa redio hiyo amesema kuwa mbali ya wao, kampeni pia
imewashirikisha wakazi wa Mwanza kwa asilimia kubwa ili kuzidi kujenga
mahusihano mazuri baina ya kituo na wananchi.
Hezron amesema 102.5 Lake Fm itahakikisha inatoa fursa kwa
wanajamii kusikika na kueleza matakwa yao ili kutafuta mikakati ya matakwa yao
kutafutiwa ufumbuzi kwa kuwa kituo redio hiyo ipo kwa ajili wananchi.
Alisema kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya 102.5 Lake
Fm kwa sasa anafanya mazungumzo na Jumuiya ya biashara
ndogo ndogo, minada na masoko ambapo maazimio yaliyofikiwa ni kuijenga ziara
maalum ya kuitembelea minada yote ndani ya jiji la Mwanza, iliyopewa
jina la Gulio la mtaa.
Alifafanua kuwa dhamira ya ziara hiyo nikusogeza elimu ya usafi
katika maeneo hayo,uboreshaji wa huduma ya vyoo minadani pamoja na maboresho ya
kimiundombinu katika minada kupitia Gulio la mtaa lakini pia litatimiza zana ya
kupeleka radio kwa wananzengo, kwa kuhakikisha inawaburudisha na muziki wa kisasa pamoja na ule
wa asilia.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'. |
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'. |
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'. |
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishangilia mara baada ya kuhitimisha kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza ijulikanayo kwa jina la 'Ng'arisha Nzengo'. |
Katibu wa wenyeviti wa Mitaa Jiji la Mwanza, Hamza Shido akishiriki katika kampeni hiyo ya 'Ng'arisha Nzengo' iliyoanzishwa na kituo cha redio cha 102 |
No comments