ZANZIBAR YAPATA UANACHAMA WA CAF, FIFA
Hatimaye Kilio cha Wazanzibara
kimepata jibu baada ya mkutano mkuu wa 39 wa Shirikisho la soka barani
Afrika (CAF) unaoendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia, umepitisha ombi la Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), kuwa mwanachama rasmi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF.
Ni jambo la kihistoria kwa
Zanzibar kwani safari hii ombi lao limepitishwa bila kupingwa na inakuwa
nchi ya 55 mwanachama wa kujitemea wa CAF.
Awali Zanzibar ilikuwa
inaunganishwa na Tanzania bara chini ya TFF na kusababisha kukosa haki za
kushiriki kama nchi kwenye mashindano yanayoandaliwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Pendekezo hilo lilipelekwa na Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF, Jamal Malinzi na
lilipokelewa na wajumbe 54 wengine waliokuwepo.
Hii maana yake ni kuwa kwa sasa
CAF ndio shirikisho mwanachama wa FIFA kwa upande wa mabara lenye
wanachama wengi zaidi kuliko wote.
Vilabu vya Zanzibar vimekuwa
vikishiriki mashindano mbalimbali ya CAF lakini kwa ngazi ya kitaifa
hawakuwa na ruhusa na walicheza kwa kuungana na Tanzania bara na
kushiriki kama Tanzania.
Kwa maana hiyo basi, chama cha
soka cha Zanzibar kitapata uwezeshaji wa kifedha moja kwa moja kutoka
CAF na FIFA kwa ajili ya timu ya taifa.
No comments