Zambia mabingwa Afrika kwa vijana chini ya miaka 20
LUSAKA, Zambia
FAINALI ya vijana wenye umri chini
ya miaka 20 ya Afrika imemalizika usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Taifa
wa Mashujaa nchini Zambia, baada ya wenyeji kuifunga Senegal mabao 2-0.
Mabao mawili yaliyowapa ubingwa
Zambia yalifungwa na Patson Daka na Edward Chilufya.
Ulikuwa ubingwa wa kwanza kwa timu
za vijana wan chi hiyo, lakini ukiwa wa pili baada ya nchini hiyo kubeba kombe
la wakubwa la Mataifa ya Afrika mwaka 2012.
Zambia ilikuwa katika kiwango bora
cha juu katika michuano hiyo ilipomaliza katika nafasi ya nne mwaka 1991, 1999
na 2001.
Ilikuwa ni mara ya pili kwa timu ya
taifa ya Senegal kucheza fainali, mara ya kwanza ilikuwa nyumbani kwao miaka
miwili iliyopita, lakini ilichapwa bao
1-0 dhidi ya Nigeria katika ardhi yao.
Kufungwa na Zambia, ni mara ya
kwanza kwa vijana wa Francois Koto, tangu mwaka 2015.
Usiku wa kuamkia leo ulikuwa wa
furaha kwa wenyeji Zambia, baada ya Patson Daka kuifungia bao la kwanza nchi
yake dakika ya 16, baada ya kipa wa Senegal, Lamine Sarr kushindwa kuudaka
mpira uliopigwa na Fashion Sakala.
Bao la pili liliwanyong’onyesha
nguvu Senegal liliwekwa wavuni dakika 35, baada ya kipa Sarr kulazimika
kuondokana langoni kwake kuuwahi mpira, lakini ulingonga Edward Chilufya, na
kutumbukia wavuni.
Nafasi ya tatu katika michuano hiyo
ilichukuliwa na Guinea baada ya kuifunga Afrika Kusini mabao 2-1 na kupata
medali za shaba.
Timu zote nne zilizocheza nusu
fainali zimekata tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka za vijana
wenye umri chini ya miaka 20, itakayopigwa nchini Jamhuri ya Korea kuanzia Mei
20 hadi Juni 11, 2017.
Ratiba ya fainali za Kombe la Dunia
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 itapangwa Jumatano Machi 15, 2017.
Wachezaji wa Zambia wakishangilia baada ya mechi dhidi ya Senagal ya fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 20 kumalizika, usiku wa kuamkia leo jijini Lusaka. |
No comments