WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) akiwasili leo Machi 17, 2017 katika Bwalo Kuu
la Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam tayari kwa ufunguzi wa
Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(wa kwanza kushoto) ni
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akisaini katika kitabu cha wageni kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(wa pili kulia) kabla ya ufunguzi wa
Mkutano huo. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa
Magereza, Gaston Sanga (wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza,
Edith Mallya.
Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kufungua rasmi
Mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Mwigulu Nchemba akiwasilisha hotuba yake kwenye Mkutano wa Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa
Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba fupi ya Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (hayupo pichani).
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza
Simon Mwanguku akiwasilisha mada katika Mkutano wa Maafisa Waandamizi
wa Jeshi la Magereza. Mkutano huo umefanyika leo Machi 17, 2017 katika
Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Brass Band ya Jeshi la Magereza kikitumbuiza kwenye ufunguzi wa huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,
Mhe. Mwigulu Nchemba(wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Wakuu wa Jeshi la Magereza Wastaafu(waliosimama mstari wa nyuma).Wa
pili kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma
Malewa, wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza,
Gaston Sanga na wa kwanza kulia ni Naibu Kamishna wa Magereza, Edith
Mallya mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi
la Magereza (Picha zote na ASP Deodatus Kazinja).
No comments