WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA LAPF,JIJINI ARUSHA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa |
Na Pamela Mollel Arusha
MFUKO wahifadhi ya wafanyakazi wa serikali za mitaa,LAPF,umeipongeza serikali kwakulipa malimbikizo ya madeni ambayo mfuko huo na mingine ilikuwa
ikiidai kwamiaka mingi na hivyo kuathiri usitawi wa mifuko hiyo..Meneja wa LAPFkanda ya kaskazini, Rajabu Kinande amesema hatua ya serikali kulipa madenihayo kumeiongezea mifuko ya hifadhi ya jamii uwezo wa kuhudumia wanachama
wao kwa wakati. Kinande, ameyasemahayo Marchi 7 jijiniArusha,alipokuwaakizungumza na vyombo vya habari kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa, AICC,kuelezea hatua yamaandalizi ya mkutano mkuu wa siku mbili wa mwaka wa wadauwaLAPF.Amesema mkutanohuo utafunguliwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, Marchi 10 mwaka huu ambapo zaidi ya wanachama 1000 wa mfuko huo wanatarajiwa kuhudhuria.Awali MenejaMawasiliano na Masoko wa LAPF,James Mloe, amesema kuwa kwenye mkutano huo kutawasilishwa mada mbalimbali zikiwemo Uendeshaji wa shughuli za mfukohuo,Hesabu zilizokaguliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG), za mwaka 2015/16ambapo mfuko huoumepata hati safi ya ukaguzi wa hesabu , uKusanyaji a michango ulipaji wa mafao kwa wanachama na uwekezaji, utawala bora na usimamizi wa uendeshajiwa mfuko huo na Raslimali fedha.
Amesema sikuya kwanza ya mkutano huo Machi 9, kwa kuzingatia kuwa ni siku ya Figo Duniani mfuko umeandaa upimaji wa figo bure kwa wanachama wote ambao utafanywa na Madaktari bingwa. Mloe amesema siku ya pili ya mkutano huoWaziri mkuu Kassim Majaliwa atazindua programu mpya ya mikopo kwa wanachama kwa kushirikiana na benki ya CRDB, iitwayo Maisha popote ambao ni mkopo wakwanza kutolewa na mfuko huo.Amesemakauli mbiu ya mwaka huu ni kuibua fursa endelevu za ajira kwa maendeleo endelevu kwa Watanzania.
Kuhusuuwekezaji kwenye viwanda,Mloe, amesema kuwa LAPF, imeweka mitaji kwenye viwanda ambako tayari wameweka hisa zao. Amesema kuwaLAPF,haiwezi kujenga viwanda na kuvisimamia uendeshaji wake bali itaweka mitaji na kusisitiza kuwa LAPF itabakia kwenye jukumu lake la msingi la kulindamichango ya wanachama wake. Mwisho .
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa kufungua mkutano wa LAPF, kesho jijini Arusha
No comments