Wanachama Wa Chama Cha Mapinduzi Watakiwa Kuwaheshimu Mabalozi
Na Pamela Mollel,Arusha
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wametakiwa kuwaheshimu mabalozi wa nyumba kumi wanaotokana na chama hicho ili kuleta maendeleo ya kasi na yenye tija kwa wananchi hali ambayo itaongeza idadi ya wanachama wapya
Pia
wanachama hao wamesisitizwa kuacha majungu badala yake kuhakikisha
wanaimarisha chama kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali sanjari na
kufungua matawi na kugawa kadi mpya kwa wakati.
Hayo
yalisemwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha, Lucia
Mwiru jijini A rusha katika Kata ya Sekei. wakati alipokuwa
akizungumza na wanachama, mabalozi wa nyumba kumi, makatibu Kata,wazee
maarufu
Alisema
yeye ni mgeni katika wilaya hiyo na ndio maana anapita kila Kata
kwaajili ya kuongea na wanachama wa CCM ikiwemo kuhakikisha kila jambo
wanalolifanya ni lazima mabalozi wa nyumba kumi waheshimiwe ikiwemo
kushirikishwa katika miradi mbalimbali ya chama.
Alikemea
vikali tabia ya baadhi ya wanachama kuwapuuza mabalozi na kuwaona
wanamaana kwenye chaguzi mbalimbali na mara ya chaguzi kuisha husaulika
kabisa
.
Aidha
alisema kuwa mabalozi ni watu muhimu sana katika chama hivyo wanahaki
ya kuhusishwa katika miradi mbalimbali ya chama ili na wao wanufaike na
keki iliyopo badala ya watu wachache kukumbatia keki hiyo
Pia
alisema baadhi ya viongozi wa ccm wanafanya miradi ya chama kama shamba
la bibi huku wanachama pamoja na viongozi wengine hawajui nini
kinaendelea na hata wakihoji wanaambiwa kuwa ni wasaliti kwa kutengezewa
maneno yasiyofaa.
Naye
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Jasper Kishumbua
alitoa rai kwa wanachama wa chama hicho Mkoa wa Arusha na kata
mbalimbali kuongeza idadi ya wanachama pamoja na kufungua matawi ili
kuongeza ari katika chama
Kwa
upande wa wanachama waliokuwepo katika mkutano huo , Nehemia Mollel na
Mariam Hussein walitoa rai kwa wanachama kujua wanachama wote wanaoishi
kwenye kila Kata ili panapotokea masuala ya uchaguzi iwe rahisi kuwajua
kwani baadhi ya wanachama wengine wanatoka Kata fulani kuja kupiga kura
kwingine na kupelekea chama kushindwa.
Picha
ikimuonyesha Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha, Lucia
Mwiru akizungumza jijini A rusha katika Kata ya Sekei. wakati
alipokuwa akizungumza na wanachama, mabalozi wa nyumba kumi, makatibu
Kata,wazee maarufu
No comments