Wadau wa muziki wa Injili kukutana wikendi hii jijini Dar es Salaam
Mtaalamu
wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo,
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Hoteli ya Lamada
jijini Dar es Salaam leo wakati akifafanua kuhusu sheria ya haki miliki
ya kazi za wasanii wa muziki.
Rais wa Tanzania Music Foundation (TMF) Dk. Donald Kassanga
akifafanua mambo kadhaa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na TMF,
kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na dawa za kulevya.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba akizungumza katika mkutano huo.
......................................
Na Christina Mseja
WADAU
wa muziki wa injili wanatarajia kukutana kesho
kwenye Kongamano la Wasanii wa muziki huo litakalofanyika katika Ukumbi
wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mtaalamu wa Sheria kutoka
Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo, alisema kongamano
hilo lina dhumuni kubwa katika kujenga uelewa kwa wasanii wa muziki
juu ya kazi zao, hususani changamoto na suluhu za kazi za Sanaa.
Kyogo
alisema kazi za Sanaa ni mali na zimekosa ulinzi na hakuna jitihada
zozote zinazoendelea katika kusaidia wasanii hao.Wasanii wamekosa
ubunifu na watu wamekata tamaa na kujiingiza katika wimbi la dawa za
kulevya. Kuwepo kwa mapungufu ya adhabu haipunguzi uhalifu kwani
wasimamizi wa sheria wanatakiwa kuwa na uwezo zaidi katika sheria hizo.
“Lazima
kuwe na sheria ya makosa ya wizi za kazi za wasanii kwani itasaidia
kupunguza wizi na itaongeza kipato na ajira, kwa kuwa muziki ni mali ya
jamii na ni afya na tiba”, alisema Kyogo.
Rais
wa Tanzania Music Foundation (TMF) Dk. Donald Kissanga aliongeza kuwa
lengo kubwa kongamano ni kuhakikisha serikali inatengeneza mazingira
bora katika tasnia nzima ya muziki jambo litakalosaidia kuongeza pato
la taifa.
“Watu
wamekuwa wakiiba kazi za wasanii na kama TMF tunalaaani na kuomba
serikali kupitia vyombo vya dola kuziba mianya hiyo" alisema Kissanga.
Katika
hatua nyingine Kissanga alisema TMF kinaungana na Serikali katika
mapambano ya dawa za kulevya nchini kwani waathirika ni pamoja na
wanamuziki na wasanii kwa ujumla.
Mwimbaji
wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba, alisema kuwa wasanii wamekuwa
wakiibiwa sana kazi zao wakati wanatumia nguvu kubwa kwa kuziandaa.
"Tuna
amini endapo Serikali ikisimamia vizuri kwa kushirikiana na TMF
wataweza kulipa kodi sawa sawa na kuendesha kazi vizuri" alisema
Ntaboba.
No comments