Header Ads

ad

Breaking News

ULAJI WA VYAKULA NA KUTOFANYA MAZOEZI WACHANGIA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA NCHINI

 Mkuu wa wilaya ya Arusha
Gabriel Daqqaro akichukuliwa vipimo  mara baada ya kuzindua wiki
ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeathimishwa katika
viwanja vya Sheikh Amri Abeid

 Muuandaaji ya wiki ya wanawake
duniani kwa mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima wa kwanza kulia
akishuhudua jinsi mkuu wa wilaya ya Arusha akiwa anachukuliwa vipimo
vya afya yake





Mgeni
Rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro akiwa
anaingia uwanjani tayari kwa  uzinduzi  Rasmi zoezi la
kupima Moyo, Cancer, Kisukari, Macho,
Magonjwa Sugu ya mfumo wa hewa Bure yanayofanyika Arusha katika Viwanja
vya Sheikh Amri Abeid  yaliyoandaliwa na Phide Entertainment kushirikiana na
wafadhili mbalimbali ambapo kilele chake ni siku ya wanawake duniani
tar 8/3/2017

Habari picha na
Woinde Shizza,Arusha
Tatizo la baadhi
ya watanzania kula vyakula bila mpangilio na kutofanya mazoezi ili kulinda afya
zao limechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa ya kisukari ,kansa,na
shinikizo la damu.
Hayo yalisemwa na
mtaalamu wa magonjwa ya yasiyoambukizwa kutoka hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt
meru,Dk Beatrice Ngogi wakati wa zoezi la upimaji wa afya bure lililofanyika
jana katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Akihojiwa na waandishi
wa habari mtaalamu huyo alisema asilimia kubwa ya kundi la watu walioathirika
na magonjwa yasiyoambukizwa ni kati ya umri wa miaka 45-60 na kudai
kuwa  mtindo wa maisha ya watu umechangia kwa kiasi
kikubwa  ongezeko la magonjwa hayo.
“mtindo wa maisha
umekuwa ni tatizo kubwa kwetu ndio maana tunawasihi watanzania tufanye
mazoezi  na kuzingatia mlo wenye
utaratibu”alisema mtaalamu huyo
Hatahivyo,mtaalamu wa
magonjwa ya kisukari katika hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani kilimanajro,DK
Valeria Matei alisema kwamba  katika siku
za karibuni watoto wadogo wanazaliwa wakiwa na ugonjwa wa kisukari mbali na
wazee ambao ilikuwa imezoeleka.
Alisema kwamba elimu ya
afya ni muhimu sana itolewe katika jamii ya watanzania kwa kuwa wengi
wanakumbwa na ugonjwa huo bila kujijua na wakishajitambua ugonjwa huo unakuwa
umeshawathiri kwa kiasi kikubwa.
Doroth Kuziwa, ambaye
ni mwathirika wa ugonjwa wa kisukari alisema ya kwamba alikuwa kubaini
kuathirika na ugonjwa huo kwa muda mrefu huku akisisitiza kwamba vyakula vya
wagonjwa wengi wa kisukari vimekuwa ghali hali ambayo inawafanya washindwe
kumudu gharama hizo.
Hatahivyo,Hiza Omary
ambaye ni mgonjwa wa macho alisema kwamba aliacha kazi ya udereva kutokana na
kusumbuliwa na matatizo ya macho huku akisema kwamba vyombo vya habari vina
jukumu kubwa la kuhabarisha umma kuhusu elimu ya afya katika
jamii.
Mkurugenzi wa kampuni
ya Phide Entertainment,Phidesia Mwakitalima alisema kwamba kampuni yake imeingia
mkataba na hospitali za KCMC  na Mt Meru
kwa lengo la kufadhili  zoezi la upimaji
wa afya bure kwa wakazi wa mkoa  wa
Arusha  katika kuelekea siku ya wanawake
duniani.
Alisema kwamba zoezi
hilo litahitimishwa siku ya kilele cha siku ya mwanamke duniani
huku akisisitiza kundi la wanawake kuzingatia
mfumo wa ulaji wa vyakula mbalimbali ili kuepuka magonjwa
yasiyoambukizwa.

 Mmoja wa madaktari wanaotoa
huduma akiwa anachukuwa damu salama kutoka kwa mwananchi ambaye
amejitolea kuchangia damu
 Mmoja wa daktari akimpongeza
mamaa mara baada ya kupimwa na kukutwa anaugongwa wa
presha
Dokta kutoka katika hospiotali ya kcmc akitoa
elimu kwa wamama waliouthuria kupata huduma ya kupimwa
bure
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro Akisaini Daftari la
Wageni la Phide Entertainment baada ya Uzinduzi wa Zoezi la kupima
buree wananchi Moyo, Cancer, Kisukari, Macho na Magonjwa sugu ya
mfumo wa Hewa .. Pamoja na changizo la Damu kwa ajili ya Ward za Wazazi
Mkoani Arusha

No comments