Header Ads

ad

Breaking News

THOMAS ULIMWENGU KUTOJIUNGA TAIFA STARS

                       Tom-Ulimwengu
Wakati timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’,kikitarajiwa kuingia kambini leo Machi 19, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam, kikiwa chini ya Kocha Salum Mayanga, kitamkosa Thomas Ulimwengu anayekipiga AFC Eskilstuna ya nchini Sweden.
Mayanga alipata taarifa hizo kutoka Sweden kuwa, Ulimwengu yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo, hicvyo hataweza kujiunga na kikosi cha Taifa Stars. 
Kutokana na kukosekana kwa Ulimwengu, Mayanga atawatumia washambuliaji Mbwana Samatta anayeichezea KRC Genk- ya nchini Ubelgiji, Ibrahim
Ajib wa Simba, Mbaraka Yusufu wa Kagera Sugar na Abdul-Rahman Mussa anayeipigia Ruvu Shooting.
Nyota wengine aliowataja Jumatatu iliyopita ni walinda milango, Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa pembeni ni Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Kessy (Yanga SC),  Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).
Mayanga aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shiza Kichuya (Simba SC).
Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati wasaidizi wake ni Kocha Wa Makipa, Patrick Mwangata, Meneja wa timu, Danny Msangi, Mtunza Vifaa Ally Ruvu wakati Daktari wa timu atakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA).

No comments