TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA OPEN HEART YA AUSTRALIA YAFANYA UPASUAJI WA MOYO
Madaktari
bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International
ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuziba matundu ya moyo
kwa mgonjwa wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo inayoendelea
katika Taasisi hiyo. Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi
leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya
hao watoto ni tisa na watu wazima wawili.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa
Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya
upasuaji wa kuvuna mshipa wa damu mguuni kwa mgonjwa wa moyo na
kuupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba kwa jina la kitaalamu
Coronary Artery Bypass Graft (CABG). Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe
12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa
upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
No comments