SIMBA SPORTS CLUB WAITIMIZA NDOTO YA DOGO WA DODOMA ALIYEANDIKA JINA LA AJIBU MGONGONI
Baada ya Messi kupata taarifa kuna mtoto ametengeneza jezi kwa mifuko ya
rambo na kuiandika jina Messi mgongoni, alimtumia jezi aliyoisaini
lakini baadae alifanya mpango wa kukutana na mtoto huyo.
March 13, 2017, kuna picha ya bwana mdogo ilikua ikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii. Picha hiyo ilimwonesha kijana mdogo akiwa ameandika hiba la mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib mgongoni mwa t-shirt yake hali iliyoashiria dogo huyo kumkubali sana nyota huyo wa Msimbazi na Taifa Stars.
Klabu ya Simba iliguswa na tukio hilo, ikapost picha ya kijana huyo na ujumbe wa kuwaomba wanaomfaham kufikisha taarifa zake kwa uongozi wa klabu ili waweze kumfikia kwa urahisi.
March 14, 2017 zimetoka taarifa kwamba, dogo huyo amepatikana na tayari uongozi wa Simba umeshatuma jezi yenye jina la Ajib kwa ajili ya kijana huyo aliyepigwa picha wakati Simba ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Hatimaye ndoto ya kijana huyu itatimia baada ya kuliweka jina Ajib mgongoni mwake.

Kama
Lionel Messi alivyoweza kuifanya ndoto ya mtoto wa Afghanstan Murtaza
Ahmadi kuvaa jezi yenye jina la Messi mgongoni mwake kuwa kweli basi
ndivyo ilivyo kwa yule dogo wa Dodoma aliyeandika jina la Ibrahim Ajib
mgongoni mwa t-shirt ilivyotimia.
Hongera kwa uongozi wa klabu ya Simba kwa kujali, ni jambo jema la mfano na la kuigwa kwenye medani ya michezo.
No comments