SERIKALI MKOANI MBEYA KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA KISHERIA ASKARI POLISI WANAOTUHUMIWA KWA WIZI WA DHAHABU CHUNYA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo katika mgodi wa dhabau wa Itumbi kata ya Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Februry 2 mwaka huu. |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Serikali Mkoani Mbeya
imeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya askari Polisi wanao tuhumiwa
kuhusika na ubebaji wa mawe ya dhahabu katika
shughuli za uokoaji wa wachimbaji waliofukiwa na kifusi mwezi February mwaka
huu Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Hatua hiyo inakuja kufuatia baadhi ya wachimbaji madini wadogo katika
mgodi wa dhahabu wa Itumbi Kata ya Matundas Wilayani Chunya kutoa malalamiko
yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla, ambaye alifika katika eneo
hilo kujionea hali halisi ya maafa hayo, ambapo inaelezwa kuwa zaidi ya
wachimbaji wadogo 25 katika mgodi wa dhahabu wa Itumbi,walifukiwa na
kifusi na kusababisha majeruhi na vifo vya watu wanne, mwezi February mwaka

Wachimbaji hao walidai mbele
ya Mkuu wa Mkoa kuwa baadhi ya
askari polisi ,walishindwa kutekeleza wajibu wao katika kufanya
kazi ya uokoaji wa watu na mali zao, badala yake wao walikimbilia kubeba mawe ya dhahabu
ambayo yalikuwa tayari yamechimbwa na wachimbaji hao, kisha kuyapakia kwenye
gari ya polisi na kuyasafirisha mahala pasipojulikana.

Wachimbaji hao, walimweleza Makalla kuwa askari
hao ambao wanadaiwa kuwa si waadilifu, wao waliendelea na shughuli ya ubebaji
wa mawe ya dhahabu ambayo yalikuwa yamechimbwa na wachimbaji na yapo nje
yakisubili kuchenjuliwa ili kupatikana madini aina ya dhahabu.

Aidha, kutokana na
malalamiko hayo, Makalla aliwataka wananchi pamoja na wachimba madini hayo kuwa
watulivu na wapole, kwa kuwahakikishia kwamba serikali italishughulikia suala
hilo na kuwachukulia hatua baadhi ya askari watakaothibitika kuhusika na tuhuma
hizo.

“Serikali
haitalinyamazia suala hili, nimeunda kikosi kazi cha watu kadhaa ambao
watayafanyia kazi malalamiko haya na kama kutakuwa na ushahidi wa bila kuacha
shaka juu ya askari kuhusika na ubebaji wa mawe ya dhahabu, basi hatua za
kinidhamu zitachukuliwa sambamba na kufikishwa mahakamani,”alisema.

Amesema, wakati zoezi
hili linafanyika, serikali imeufunga mgodi huu wa Itumbi, na kuwataka
wachimbaji kutofanya shughuli yoyote kwani mbali na maafa yaliyotekea pia mgodi
huo umeghubikwa na changamoto nyingi, ukiwemo mgogoro baina ya wananchi na
mfanyabiashara Vicent Minja juu ya nani mmiliki halali wa eneo la mlima huo
unaosemekana kuwa na madini aina ya dhahabu.

Mmoja wa wachimbaji wadogo wadogo katika mgodi wa Itumbi kata ya Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya akitoa malalamiko yake mbeya ya Mkoa wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (hayupo Pichani). |
Mkutano ukiendelea. |
No comments