Rais Magufuli azindua mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme
Rais John Pombe Magufuli, amelipongeza
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kutokana na kasi yake ya kusambaza
umeme nchini hususan vijijini.
Rais aliyasema hayo Machi 5, 2017
wakati akizindua Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme
wa 132kv mkoani Mtwara.
Mradi huo utakamilika Mei 30, 2017 na
kitahudumia mikoa ya Mtwara na Lindi na hivyo kutatua kero ya
upatikanaji umeme kwenye mikoa hiyo ambayo shughuli za kiuchumi
zimeongezeka sana. Awali kituo hicho kwa sasa kina uwezo wa 33kv.
“TANESCO mmenifurahisha sana kwa
kutekeleza vema ilani ya uchaguzi ya CCM, kwa kuhakikisha wanachi kote
nchini wakiwemo wa vijijini wanapatiwa umeme,” alisema.
Rais pia alisema, anatambua changamoto zinazolikabili shirika hilo hususan madeni ya bili za umeme kwenye taasisi za serikali.
“Ninaagiza, wale wote wanaodaiwa bili za umeme na TANESCO, walipe madeni yao haraka, vinginevyo muwakatie umeme,” alisema Rais.
“Hata Ikulu kama inadaiwa we kata,
najua pia kuna deni la shilingi Bilioni 162 Kule Zanzibar, nako kama
hawatalipa kateni umeme. tunataka TANESCO iharakishe kusambaza umeme kwa
wananchi sasa wasipolipwa madeni watawezaje kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi?,” aliuliza Rais Magufuli.
Aidha kutokana na kufurahishwa na kasi
ya TANESCO kusambaza umeme kwenye maeneo Mengi ya nchi, amesema ofisi
yake iko tayari kusaidia fedha pale itakapoonekana kuna mkwamo wa
kifedha katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya umeme.
Rais
Magufuli(wapili kushoto), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt.Alexander Kiaruzi, na Mwenyekiti wa
CCC mkoa wa Mtwara, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo hicho.
Rais akiandika kitu, wakati akiteta na Profesa, Muhongo wakati wa uzinduzi huo.
Rais Magufuli akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO baada ya kupiganao picha.NA K-VIS BLOG
No comments