PROF.MUHONGO -ASISITIZA MKOA WA PWANI KUPEWA KIPAOMBELE CHA UMEME KUTOKANA NI UKANDA WA VIWANDA
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
(mwenye fulana ya Bluu) na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakifukia
nguzo ya umeme kwa udongo ikiwa ni ishara ya kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa
Usambazaji Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani.
(mwenye fulana ya Bluu) na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakifukia
nguzo ya umeme kwa udongo ikiwa ni ishara ya kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa
Usambazaji Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani.
Watendaji kutoka kampuni ya Steg
International Services wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini (hayupo
pichani), wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
katika mkoa wa Pwani. Kampuni hiyo itatekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo wa
Awamu ya Tatu.
International Services wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini (hayupo
pichani), wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
katika mkoa wa Pwani. Kampuni hiyo itatekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo wa
Awamu ya Tatu.
Mwamvua Mwinyi, Pwani
WAZIRI
wa nishati na madini, Profesa Sospeter Muhongo,amezindua mradi wa umeme
vijijini (REA)awamu ya tatu katika mkoa wa Pwani na kudai mkoa huo
utapewa kipaombele kwani ni kimbilio la wawekezaji na ukanda wa viwanda.
Aidha amewataka watanzania kuacha kujidharau kupitia mradi huo kutokana ni mkombozi wa wananchi .
Mbali
ya hayo, Profesa Muhongo anasema,mwaka 2007 kulikuwa na asilimia 2 pekee ya
watumiaji wa nishati ya umeme lakini kwa sasa kasi inakua ambapo
imefikia asilimia 49.5.
Akizindua
awamu ya tatu ya mradi huo na kumtambulisha mkandarasi kutoka Tunisia
kampuni ya Steg katika mkoa huo,alisema ni wakati wa kuchangamkia fursa
hiyo kwa kila mtanzania mwenye mahitaji ya umeme.
Alisema
katika awamu hiyo,imetengwa kiasi cha sh.trilioni moja ambapo vijiji
3,559 vitafikiwa nchini na mkoa wa Pwani vitafikiwa vijiji 150
vilivyokuwa havijafikiwa kwenye awamu ya kwanza na ya pili.
“Malengo
yetu ni kuvifikia vijiji vyote 12,268 nchini ,kwa kutumia umeme kupitia
Tanesco na mradi huu wa umeme vijijini ili kila mmoja anufaike nao na
kuondokana na kutumia vibatari”alisema.
Hata
hivyo ,Pro.Muhongo alisema, wakati mradi wa REA awamu ya tatu ukianza
katika maeneo mbalimbali nchini ni lazima upelekwe katika taasisi
ikiwemo zahanati,shule na madhehebu ya dini .
Alisema mkoa wa Pwani ni mkoa kati ya mikoa iliyojikita katika viwanda na uwekezaji hivyo ni lazima nguvu kubwa ielekezwe huko.
Pro.Muhongo
alimtaka mkuu wa mkoa wa Pwani kuwaweka tayari wataalamu wake wa
mkoa,na wataalamu wa Tanesco ,REA,wabunge na meneja wa kanda ,ili kuweza
kubainisha mahitaji yote ambayo yatarahisisha kufanyiwa kazi na wizara.
Aliwaomba
wananchi watakaopitiwa na miundombinu ya umeme vijijini kutotaka fidia
ili serikali iweze kufanikisha malengo yake na kuinua maendeleo ya
watanzania.
Pro.Muhongo
alisema kuwa fedha zilizotengwa ambazo ni karibu trilioni moja
zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo hazitakuwa sehemu ya fidia kwa ajili
ya maeneo umeme huo utakapopita.
“Bajeti iliyopangwa kutumika kwenye awamu hii kwa nchi nzima ni mara tatu ya bajeti iliyopita
huku fedha hizo zikiwa ni za ndani hivyo wananchi wajitolee pasipo kudai fidia,” alisema.
Waziri
huyo,alieleza kwamba,serikali imedhamiria kufikisha umeme kwa
watanzania ,kwa malipo yenye gharama nafuu ya.sh.27.000 sawa na majogoo
mawili.
Pro.Muhongo,alimpongeza
mkuu wa mkoa wa Pwani,kwa kukuza sekta ya viwanda na uwekezaji, pamoja
na mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na wa Kibaha Vijijini Hamoud
Jumaa kwa kupigania maendeleo ya majimbo yao.
Nae
mkurugenzi wa REA, Gisima Nyamo-Hanga alisema moja ya
changamoto zinazowakabili ni baadhi ya wananchi kudai fidia kwa maeneo
ambayo miundombinu ya umeme inapitishwa.
Mkuu
wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema kuwa mkoa huo
unakabiliwa na changamoto ya wateja kuhitaji kuunganishiwa umeme lakini
vifaa kama vile nguzo, mita na nyaya ni vichache.
Ndikilo
aliomba mkoa huo uongezewe nguvu ya umeme megawatt 60 ambapo kwasasa
wanapata megawati 38 hadi 40 ambazo hazikidhi mahitaji ukizingatia mkoa
umesheheni viwanda.
Kwa
upande wake Mbunge wa Chalinze, alieleza
mahitaji ya umeme ni makubwa katika vijiji vilivyopo Chalinze .
Aliomba mahitaji mapya yaingizwe kwenye bajeti kwa lengo la kufanyiwa kazi katika bajeti ya 2017-2018.
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa alisema kuwa baadhi ya vijiji
kama Gwata, Lukenge, Mpiji na baadhi ya misikiti, shule na zahanati havina
umeme hivyo kushindwa kujiendeleza.
No comments