OPERESHENI YA VIROBA YAFUMANIA KIWANDA CHA NYATI SPRIT KUWA VIROBA
Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Utekelezaji
wa operesheni hiyo umeanza kufanyika leo baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipotangaza
marufuku hiyo Februari 20 juu ya vileo vilivyo katika vifungashio
viondoke katika mzunguko wa biashara na watengenezaji wahamie katika
mfumo wa chupa kwa kuanzia milimita 250.
Operesheni
ya kukamata viroba imeanza leo jijini Dar es Salaam ikisimamiwa na
Ofisi ya Makamu wa Rais Katika Kiwanda cha Kampun ya nyati spirit
kilichopo Vingunguti ambapo katoni za viroba 7067 aina ya nyati zimekutwa katika kiwanda hicho.
Akizungumza
katika operesheni Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Dawa na
Chakula (TFDA ), Emmanuel Alphonce amesema operesheni imeanzia jiji la
Dar es Salaam na kesho itaendelea nchi nzima chini ya Kamati za Ulinzi
na Usalama za Wilaya na Mikoa
Mkurugenzi
wa kiwanda hicho Rupa Suchik amesema hatatengeneza tena viroba ikiwa ni
agizo la serikali na vilivyopo watateketeza . Amesema
kuanzia jana ameshapunguza wafanyakazi 150 kutoka 300 kutokana na agizo
hilo na hao wataingia katika mfumo wa uzalishaji vileo katika mfumo wa
Chupa.
Meneja
wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA ), Emmanuel
Alphonce akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya
operesheni ya viroba katika kiwanda cha nyati sprit leo Vingunguti
jijini Dar es Salaam.
Vijana
wakipanga Viroba katika boksi walipokutwa na timu ya operesheni viroba
iliyofika katika kiwanda cha Nyati Spirit leo jijini Dar es Salaam.Picha
na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Sehemu ya Katoni za Viroba vilivyokutwa katika kiwanda cha nyati sprit leo jijini Dar es Salaam.
Mafisa
wa serikali wakikagua nyaraka mbalimbali za kiwanda cha Nyati Sprit
ikiwa ni uhalali wake wa kuendelea kufanya biashara katika mfumo mpya
kutoendelea.
No comments