Ngoma, Tambwe, Kamusoko tayari kuivaa Zanaco
Amis Tambwe na Donald Ngoma |
WAKATI wapinzani wao Zanaco FC kutoka Zambia wakitaraji kuingia nchi
saa kumi jioni leo Alhamisi wachezaji Donald Ngoma, Amis Tambwe, Juma
Abdul, Thaban Kamusoko wote wameanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa
Jumamosi hii katika Caf Champions League.
Awali wachezaji hao walizua hofu ya kuukosa mchezo huo wa kwanza
hatua ya mwisho kabla ya kufuzu kwa hatua ya makundi kutokana na
majeraha yaliyokuwa yakiwakabili. Daktari wa Yanga SC,Dk. Bavu
amethibisha kuwa wachezaji hao wanaweza kucheza mchezo huo isipokuwa
mlinda mlango Beno Kakolanya na beki Pato Ngonyani pekee.
“Wachezaji wote waliokuwa na majeraha walianza mazoezi Jumatano
hii, isipokuwa wawili Beno Kakolanya na Pato Ngonyani ambaye
alikuwa na malaria na wanaendelea na matibabu, lakini wengine wote
wameanza mazoezi. Mashabiki wa Yanga waondoe wasiwasi kwa sababu
Tambwe, Ngoma na Kamusoko wote wapo vizuri na wanaweza kutumika katika
mchezo wa Jumamosi ikiwa watapewa nafasi na benchi la ufunzi,” anasema
Dk. Bavu.
No comments