Mwanasheria Tundu Lissu akamatwa na Jeshi la Polisi
Tundu Lissu |
Taarifa ambayo imetolewa na Afisa
Habari wa Chadema, Tumaini Makene imesema kuwa Tundu Lissu amekamatwa
wakati akitoka Mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili ya
uchochezi.
“Mwanasheria Mkuu wa Chama Tundu
Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi muda mfupi uliopita na anashikiliwa
Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) jijini Dar es Salaam. Hadi sasa
polisi hawajasema sababu ya kumkamata na kumshikilia Tundu punde tu
baada ya kutoka Mahakama ya Kisutu ambako kesi dhidi yake kuhusu tuhuma
za uchochezi ilikuwa imefutwa na mahakama hiyo.” imesema sehemu ya taarifa ya Makene.
No comments