MWANAMME AJIUA KWA KUNYWA SUMU KISA WIVU WA MAPENZI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando |
Pamoja na vifo hivyo, mkazi wa kitongoji cha Mafulala, Manispaa ya
Sumbawanga, Joel Mwenga (48), anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za
kuteketeza kwa moto nyumba ya Maria Kakoko (26) kwa wivu wa mapenzi.
Taarifa za awali za Polisi zinaeleza kuwa, Gervas alichukua uamuzi wa
kujiua kwa sumu baada ya kukataliwa na mkewe Maria Mtete (35) ambaye
alimtaka mume huyo ampatie talaka kwa kuwa amempata mwanaume mwingine
ambaye ni wa rika lake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, amethibitisha tukio hilo
na kueleza kuwa ni la usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Isasa,
wilayani Nkasi. Alisema Gervas alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu
katika Kituo cha Afya katika kata ya Kirando, mwambao mwa Ziwa
Tanganyika wilayani Nkasi.
“Mzee huyo alikunywa sumu ambayo haijajulikana mara moja, aliamua
kukatiza maisha yake kwa kuchukua uamuzi huo baada ya kukataliwa na
mkewe (Maria Mtete) ambaye alidai waachane kwa kuwa alikuwa amepata
mwanaume mwingine,” alieleza Kamanda.
Alisema mwili umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Kituo cha Afya
cha Kirando kwa uchunguzi ili kubaini aina ya sumu aliyokunywa. Aidha,
Kamanda alisema mke wa marehemu alitoroka baada ya tukio hilo.
Katika tukio jingine kwenye kitongoji cha Kaloleni mashambani kijijini
Kate wilayani Nkasi, Andrew Matandiko (16) alikufa baada ya kupigwa na
radi juzi saa 4:00 mchana.
Katika tukio la moto, Kamanda Kyando alisema Mwenga anashikiliwa na
polisi kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya Kakoko kwa moto. Alisema tukio
hilo ni la Machi 05, mwaka huu saa 5:30 usiku. Kamanda alisema chanzo ni
wivu wa mapenzi.
Chanzo-Habarileo
No comments