MWAMUZI AONDOLEWA LIGI KUU YA VODACOM
Mwamuzi wa kati, Ahmada Simba |
KAMATI ya Bodi ya
Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi za Tanzania (Kamati ya Saa 72), imemwondoa
Mwamuzi wa kati, Ahmada Simba katika orodha wa waamuzi watakaochezesha mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2016/2017.
Hatua hii imefikiwa baada
ya utetezi wa Mwamuzi Simba kudai kwamba, hakuona tukio la Mchezaji wa Yanga, Obrey Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa
na kumwonya mchezaji kwa kadi ya njano.
Tukio hilo lilitokea
katika mchezo ambao Yanga walikuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye
Uwanja wa Taifa, Machi mosi, mwaka huu.
Katika hiyo ya njano
ilikuwa ni ya kwanza kwa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 imeifuta
kadi hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa
kutolewa kwa Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.
Kadi hiyo ilikuwa ni
msingi wa kadi nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena
kwa kadi ya njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.
Kufutwa kwa kadi ya njano
ya kwanza, kunasababisha kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wa kadi hiyo
ulisababisha kadi nyekundu hivyo, mchezaji angepaswa kukosa mchezo mmoja. Hata
hivyo, kadi ya pili ya njano inahesabiwa.
Uamuzi mwingine
ulikuwa ni kuipiga faini Yanga iliyocheza na Simba Februari 25, 2017
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Wanajangwani hao kuingia
uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.
Kitendo hicho ni kwenda
kinyume cha kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia
uwanjani kwa kutumia milango rasmi. Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya
Ligi Kuu, Kamati imeipiga Yanga fainali ya Sh 500,000 (lakini tano).
No comments