MONACO, LEICESTER CITY ZATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA
Tiomoue Bakayoko akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la tatu dhidi
ya Manchester City usiku wa kuamkia leo mjini Monaco.
|
Timu ya Monaco ya Ufaransa usiku wa kuamkia leo imefabnikiwa kuitoa kwenye mashindano ya Klabu ya Bingwa timu ya Man City ya England kwa kuichapa mabao 3-1 katika mchezo uliofpigwa nchini Ufaransa na kufanikiwa kuingia hatua
ya robo fainali.
Ushindi huo umeiwezesha Monaco kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-6, lakini mabao ya ugenini yameibeba
Monaco ambayo ilifungwa 5-3 jijini Manchester katika mechi ya kwanza.
Monaco walipata mabao mawili ya haraka katika kipindi cha kwanza kupitia Mbappe Lottin na Fabinho, yaliyodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Leroy
Sane aliwapa furaha ya muda mfupi mashabiki wa Man City kwa kufunga bao dakika ya 71, lakini dakika ya 77, Tiomoue Bakayoko akazima shangwe zao kwa kufunga bao la tatu lililoiwezesha Monaco ambao walikuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Stade Louis II.
Katika mechi nyinine, Juventus ilikata tiketi ya kucheza robo fainali baada ya kuichapa FC Porto bao 1-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-0, huku mabingwa wa England,
Leicester City ikiingia robo fainali kwa kuilaza Sevilla mabao 2-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2.
Mechi nyingine ilikuwa kati ya Atletico Madrid dhidi ya Bayer Leverkusen ambo ulimalizika kwa suluhu. Atletivo imesonga mbele kwa jumla ya mabao 4 - 2.
No comments