MECHI YA YANGA DHIDI YA ZANACO KESHO, AZAM FC DHIDI YA MBABANE JUMAPILI
Yanga |
Maandalizi yote kwa michezo miwili ya kimataifa, yamekamilika.
Michezo hiyo ni kati ya Young Africans ya Tanzania na Zanaco ya
Zambia utakaochezwa Jumapili kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika pia Azam
FC ya Tanzania na Mbabane Swalows ya Swaziland kuwania Kombe la Shirikisho
barani Afrika.
Kwa upande wa Young Africans dhidi ya Zanaco, mchezo huo
utafanyika Jumamosi Machi 11, mwaka huu. Waamuzi kutoka Djibouti
ndio watakaochezesha mechi hiyo.
Waamuzi hao ni Djamal
Aden Abdi ambaye atapuliza kipenga wakati wasaidizi wake ni Hassan Yacin na
Farhan Salime ilihali mwamuzi wa akiba atakuwa Souleiman Djamal. Kamisha katika mchezo huo
Na. 61 atakuwa Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.
Kiingilio katika mchezo
huo kwa mujibu wa Mratibu wa Mechi za Kimataifa wa Young Africans, Mike Mike ni
Sh 20,000 kwa VIP ‘A’, Sh 10,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ na Mzunguko (Viti vya Rangi
ya chungwa, kijani na bluu) ni Sh 3,000.
Azam wao watacheza
Jumapili Machi 12, mwaka huu na Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa
Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Waamuzi watakochezesha
mchezo huo wanatoka Benin ambao ni Mwamuzi wa kati, Addissa Abdul Ligali na
wasaidizi ni Medegnonwa Romains Agbodjogbe na Babadjide Bienvenu Dina huku
Mwamuzi wa akiba akiwa Moumouni Kiagou na kamisha wa mchezo atakuwa Mohamed
Omar Yusud wa Kenya.
Kiingilio katika mchezo
huo kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ni Sh 10,000 kwa VIP,
Jukwa Kuu itakuwa ni Sh 5,000 na Mzunguko itakuwa ni Sh 3,000.
Wakati huohuo, tiketi za
waamuzi wa Tanzania walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),
kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu za AS Porto Louis 2000
ya Mauritius na El Hilal ya Sudan wikiendi ijayo, wamepata tiketi zao za
kusafiri.
Katika mchezo huo ambao
utafanyika ama Machi 17, 18 au 19 Mwamuzi wa kati atakuwa Israel Mujuni Nkongo
wakati wasaidizi wake watakuwa ni Samuel Hudson Mpenzu na Josephat Deu Bulali
huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Hery Sasii. Kamisha katika mchezo huo Na. 78
atakuwa Jerome Kelvyn Damon kutoka Afrika Kusini.
Azam FC |
No comments