Malinzi kufunga kozi ya makocha leo
Tanzania
Football Federation
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA
Karume Memorial Stadium, Uhuru / Shaurimoyo Rd
P.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania .
Telefax: + 255-22-2861815
|
|
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kesho Jumatatu, Machi 13, 2017 anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya ‘Intermidiate’
kwa makocha 27 wanaotarajiwa kuhitimu.
Kozi hiyo iliyoendeshwa na Wilfred
Kidao - Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),
itafungwa saa 5.00 asubuhi kwenye Viwanja vya Michezo vya Bandari, vilivyoko
Tandika jijini Dar es Salaam.
Mbali ya Kidao, wakufunzi wengine
walikuwa ni Manyika Peter aliyefundisha programu au mtaala kwa makocha wa
makipa; Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyewanoa makocha hao kuhusu tiba za
wanamichezo/wanasoka na Mkufunzi wa muda mrefu wa soka, Hemed Mteza.
Wanafunzi wa kozi hiyo wanaotarajiwa
kuhitimu kesho Jumatatu ni pamoja Doris Malyaga ambaye ni Mwanamke pekee kati
ya wanafunzi 27 walisoma kozi hiyo kwa kipindi cha siku 14 cha mwanzo wa mwaka.
Doris ni mwanahabari za michezo aliyehudhuria kozi hiyo. Anaandikia gazeti la
MwanaSPOTI linalotolewa na Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi (MCL).
Wengine ni nyota wa zamani wa timu ya
mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliopata kuchezea klabu kongwe na
kubwa nchini. Wanafunzi hao ni Boniface Pawasa, Fred Mbuna, Innocent Haule,
Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na Mussa Hassan Mgosi.
Wengine ni Omar Kapilima, Amosi Mgisa,
Uhuru Mwambungu, Yussuf Macho, George Minja, Haruna Adolf, Selemani Omari, Ally
Ruvu, Masoud Selemani, Haji Mustapha, Mhasham Khatib, Issa Ndunje, Salum
Kapilima, Said Salum, Julio Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde
na Evod Mchemba.
|
|||||
No comments