MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MBABANE SWAZILAND LEO KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua gwaride la
Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili kwenye
Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo
march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na
serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu
wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia vikundi vya
Burudani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme
Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march,16, 2017 kwa ajili ya
kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya maendeleo
kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili Heshima
kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane
Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa
nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo
Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya
viongozi wa Swaziland alipowasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme
Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya
kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo
kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
…………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane –
Swaziland leo 16-Mar-2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa
nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mara baada ya kuwasili katika
uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini Mbabane – Swaziland,
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi
mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa Serikali
ya Swaziland Owen Nxumalo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo amekagua gwaride la heshima
lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia vikundi mbalimbali vya
burudani uwanjani hapo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN
POMBE MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na
Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye mkutano huo.
Hapo kesho tarehe 17-Marchi-2017,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa Asasi ya Siasa,
Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika ambao utajadili
kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.
Mkutano huo wa SADC Double Troika
utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati
Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar es Salaam tarehe 24
februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya kuitisha
mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye hizo.
Mkutano wa SADC Double Troika
utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi hiyo ambazo ni
Tanzania,Swaziland, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.
Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dakta Augustine
Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbabane – SWAZILAND.
No comments