Header Ads

ad

Breaking News

MADAKTARI WATAKIWA KUWA TAYARI KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI DHIDI YA VITENDO VYA UNYANYASAJI KIJINSIA

index
Na Masanja Mabula -Pemba ..
 
MADAKTARI kisiwani Pemba wametakiwa kuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani juu ya vitendo vya udhalilishaji vinavyoendelea siku hadi siku dhidi ya wanawake watoto, ili wasipoteze muelekeo wa kupata fursa za kiuchumi nchini.
Hayo yalielezwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Pemba Khadija Khamis Rajab katika hospitali ya Wete, ikiwa ni shamra shamra ya siku ya wanawake duniani.
Alisema kuwa, iwapo wanawake na watoto watadhalilishwa ndoto zao hukatika na kutofikia malengo aliyoyakusudia yanayoweza kumpatia fursa za ajira katika kujiimarisha kiuchumi.
Afisa huyo alisema kuwa, zipo kesi ambazo madaraktari wanahusika na udhalilishaji kwa wanawake na watoto na kuwataka kuwa mstari wa mbele katika kutoa ushahidi wa vipimo mahakamani pindi unapotokea udhalilishaj huo.
Hata hivyo alipongeza juhudi zinazofanywa na baadhi ya madaktari akiwemo Sauda Kassim wa hospitali ya Chake Chake kutokana na kuwa mstari wa mbele kutetea na kutoa ushahidi wa kutosha mahakamani na kumuhudumia muathirika ipasavyo.
 Kwa upande wake daktari msaidizi katika hospitali hiyo, Kulthum Bakar Juma, ameeleza kuwa kutokana na udhalilishaji wanaofanyiwa mahakamani pamoja kuona watuhumiwa wanaachiwa huru bila kutiwa hatiani linawarudisha nyuma madaktari katika kutoa ushahidi mahakamani.
 Nae Daktari Asya Omar Abrahman kutoka kitengo cha Benki ya Damu katika hospitali hiyo amesema, wamekuwa wakipoteza muelekeo wanapotakiwa kutoa ushahidi mahakamani, kwani mwisho wa siku mtuhumiwa anaonekana mitaani na kurudia tena udhalilishaji bila ya kuogopa.
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8, ikiwa ujumbe wa mwaka huu unasema ‘imarisha fursa za ajira kumuwezesha mwanamke kiuchumi’.

No comments