LUGALO YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MCHEZAJI WAKE UGANDA
Mshindi wa Divisheni A Nett mashindano ya Enntebe Ladies Open 2017 kutoka Klabu ya Lugalo, Vicky
Elias akiwa katika harakati ya mchezo huo katika michuano iliyofanyika
Uganda hivi karibuni.
Mshindi wa Divisheni A Nett
Mashindano ya Enntebe Ladies Open 2017 kutoka Klabu ya Gofu ya Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika
harakati ya Mchezo huo katika Michuano iliyofanyika Uganda Hivi
Karibuni.
Bingwa Mashindano ya Wachezaji wa
Ridhaa ya Moshi Mwaka 2016 Nicholous Chitanda akiwa katika harakati
za mchezo huo.( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
…………..
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Klabu ya Gofu ya jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo imejivunia kuanza vyema mwaka 2017 baada ya Mchezaji wake Vicky Elias kuibuka na ushindi wa Divisheni A Nett katika Mashindano ya Wanawake Enntebe Ladies Open yaliyomalizika hivi Karibuni nchini Uganda.
AKizungumza na Waandishi wa habari mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu
Michael Luwongo alisema Ushindi huo ni ishara tosha ya Mafamikio ya
Kimchezo kwa mwaka 2017 kwani alikuwa mtanzania pekee kati ya Wachezaji
53 walioshiriki.
”
Unajua tunajipanga kimataifa na tuliahidi kuweka nguvu katik mashindano
kimataifa ,kwa mwaka 2017 na huu ndio mwanzo hivyo mashabiki wa Lugalo
na Wanachama wajipange kufuarahia Timu yao kutokana na mafanikio
yatakayopatikana kimataifa.
Aliongeza kuwa licha ya matokeo ya Kimataifa pia Michezo yeyote ambayo Timu
ya Gofu ya Lugalo itaalikwa basi watahakikisha wanafanya vyema ili
adhama ya Timu ya Gofu ya Lugalo kuwa Timu Bora inatimia.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa ushindi wa Vicky ni Ushindi Mkubwa kutokana na
Maandalizi pamoja na Washiriki waliojitokeza kushiriki michuano hiyo
lakini ni sifa kwa Nchi kw sababu mbali na kutoka Klabu ya Lugalo lakini
kubwa zaidi ni Mtanzania.
Kwa
Upande wake Vicky Elias alisema mashindano yalikuwa magumu lakini
alipambana kufa na kupona kurejesha heshima ya Klabu na Nchi kwa Ujumla
na kufanikiwa kurejea na ushindi ambao haikuwa rahisi kwani siku ya
kwanza alipiga mikwaju 83 na kutoa kiwango chake cha uchezaji ambacho ni
Tisa.
Katika siku ya pili ya mashindano hayo Vicky aliibuka na Mikwaju ya Jumla 81 baada ya kutoa kiwango chake cha Uchezaji cha Tisa na hivyo kuibuka na Ushindi wa Kwanza Divisheni A na kuwashinda Wachezaji Wenzake kutoka Uganda na Kenya waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Wakati huo huo kufuatia
Maandalizi ya mashindano ya wachezaji wa Ridhaa nchini Tanzania Amature
Stoke Play yanayotarajiwa kufanyika Moshi mkoani Kilimanjaro machi 12 Wachezaji wa Timu ya Lugalo wanaendelea na Mazoezi kujiwinda na Michuano hiyo.
Bingwa mtetezi wa mashindano ya hayo kutoka Lugalo Nicholous
Chitanda amesema yuko katika maandalizi kujiandaa na michuano hiyo ili
kutetea Ubingwa wake alionyakua mwaka jana ili kuhakikisha unabaki
katika Klabu ya Lugalo.
No comments