KABUNDA WA MWADUI MCHEZAJI BORA WA FEBRUARI
Mchezaji wa timu ya
Mwadui FC, Hassan Kabunda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom wa mwezi Februari kwa msimu wa 2016/2017.
Kabunda aliwashinda wachezaji Laudit Mavugo wa Simba SC na
Ibrahim Ajib pia wa Simba SC.

Katika mechi tatu ambazo Mwadui ilicheza kwa mwezi huo, Kabunda
alicheza kwa dakika zote 270 na kuisaidia timu yake kukusanya jumla ya pointi
sita zilizoifanya ipande kwa nafasi mbili katika Msimamo wa Ligi kwa mwezi huo
wa Februari (kutoka nafasi ya nane hadi ya sita).
Kabunda alifunga jumla ya mabao manne katika mechi hizo tatu
kati ya sita iliyofunga timu yake. Kiungo huyo mshambuliaji alionesha nidhamu
ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la mdomo au kadi kutoka kwa waamuzi.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Kabunda atazawadiwa kitita cha sh.
1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo, kampuni ya Vodacom
Tanzania.
No comments