John Barnes awasili Nchini Kuhudhuria Mashindano ya Standard Chartered
Akiwa
nchini Barnes atafanya mafunzo kwa timu ya taifa ya vijana chini ya
miaka 15 Serengeti Boys pamoja kuhudhuria fainali za mashindano ya
Standard Chartered road to Anfield ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 100 ya benki hiyo yatakayofanyika Jumamosi Machi 4.
Bingwa wa Mashindano hayo atapata nafasi ya kwenda nchini Liverpool Uingereza.
Timu zilizoingia fainali za mashindano hayo ya kikanda ni Azania Group ya Tanzania, Capital FM ya Kenya na Cocacola ya Uganda.
Mchezaji
nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (wa pili kushoto)
akiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere- VIP
Terminal I na kupokelewa na wenyeji wake ambao ni Mkuu wa Idara ya Fedha
wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (wa pili kulia), Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba (kulia) pamoja na
Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas (kushoto).
Mchezaji
nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (wa pili kulia) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wenyeji wake Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki
ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (kulia), Mkuu wa Mahusiano na
Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba (wa tatu kulia) pamoja na Afisa
Habari wa TFF, Alfred Lucas (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere- VIP Terminal II
leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Mchezaji nguli wa
kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mchezaji
nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes akionyesha jezi ya
Timu ya Taifa kwa waandishi wa habari aliyokabidhiwa na Afisa Habari wa
TFF, Alfred Lucas mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mchezaji
nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (katikati)
akiongozana na wenyeji wake Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard
Chartered, Abdulrahaman Said (kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa
benki hiyo, Juanita Mramba (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es
Salaam.
Mchezaji
nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (wa pili kulia)
akizungumza jambo na Meneja wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam-The
Kilimanjaro, Timothy Mlay alipowasili kwenye hoteli hiyo jioni hii
jijini Dar es Salaam.
Mchezaji
nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes akisalimiana na mmoja
wa mashabiki wa timu ya Liverpool Benjamin Kasenyenda mara baada ya
kuwasili kwenye wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam-The
Kilimanjaro.
No comments