Hatimaye Godbless Lema achomolewa kwa dhamana
ARUSHA: Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Machi 3, 2017 imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA).
Katika kesi hiyo iliyotolewa
maamuzi majira ya saa 7:30 mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini
baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana hiyo
kwa masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni
tatu.
Lema amekaa mahabusu kwa
takribani miezi minne sasa tangu alipokamatwa mwezi Novemba mjini Dodoma
na kusafirishwa kupelekwa Arusha kisha kufunguliwa kesi ya uchochezi.
No comments