Header Ads

ad

Breaking News

Chelsea yaituliza Manchester United Kombe la Ligi

LONDON, England
Antonio Conte amekuwa bora mara mbili dhidi ya Jose Mourinho msimu huu, baada ya Chelsea kuifunga Machester United iliyokuwa na wachezaji 10 bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Stamford Bridge na kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Chama cha Mpira wa Miguu England (FA Cup), jana.

N'Golo Kante, aliipeleka Chelsea nusu fainali dakika ya 51, na kuzima ndogo za wageni wao baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu Ander Herrera dakika ya 35, akionesha kadi ya pili ya njano, kwa kumchezea vibaya Eden Hazard.
Kinara huyo wa Ligi Kuu Bara, Chelsea atakwenda Wembley kuumana na majirani zao pale London, Tottenham Hotspur, wakati nusu fainali nyingine itawakutanisha Arsenal na Manchester City.
United, ambao watashuka uwanjani Alhamisi dhidi ya Rostov ya Urusi katika Ligi ya Europa hatua ya 16 bora, iliwakosa Zlatan Ibrahimovic na majeruhi Wayne Rooney.
Kocha Jose Mourinho wa Manchester United na Antonio Conte wa Chelsea wakirushiana maneno kwa mara ya pili msimu huu baada ya Herrera kutolewa nje kwa kuonesha kadi ya pili ya njano katika mchezo wao usiku wa kuamkia leo.

Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson (kulia), akishuhudia mechi hiyo akiwa na Mtendaji mkuu wa zamani wa Man United, David Gill.


Kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate, akifuatilia mechi ya Chelsea dhidi ya Man United usiku wa kuamkia leo, ikiwa ni maandalizi ya kikosi chake cha taifa kitachocheza na Ujerumani na Lithuania.
N’goro Kante na wachezaji wenzake wa Chelsea, Eden Hazard na Cesar Azpilicueta wakishangilia bao lililofungwa na Kante.

Kiungo wa zamani wa Manchester United, David Beckham akiangalia mechi kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.


Kiungo wa Chelsea, Willian akimiliki mpira mbele ya Marcos Rojo (kushoto) na Darmian wa Manchester United usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London. Chelsea ilishinda bao 1-0.

Beki wa Chelsea, Azpilicueta na kiungo wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan wakiwania mpira.

No comments