Bayern Munich yaididimiza Arsenal 5-1, yatinga robo fainali kwa jumla ya mabao 10-2
Theo Walcott akiifungia Arsenal bao
dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya
Klabu Bingwa Ulaya iliyopigwa usiku wa kuamkia leo jijini London.
|
|
Kiungo Arturo Vidal, akishangilia baada ya kuifungia Bayern Munich bao la nne na tano. |
MABINGWA
wa soka nchini Ujerumani, Bayern Munich usiku wa kuamkia leo imeididimiza
Arsenal ya England mabao 5-1, katika mechi ya Klabu Bingwa Ulaya iliyopigwa
Uwanja wa Emirates jijini London, hivyo imesonga mbele kwa jumla ya mabao 10-2.
Katika mechi ya kwanza, Arsenal
ikiwa ugenini ilisalimu amri kwa kupigwa mabao 5-1 na kuweka historia katika
michuano hiyo ya kufungwa mabao yenye idadi sawa katika mechi zote mbili.
Arsenal walianza mchezo huo kwa
kuonesha nia ya kulipa kisasi, baada ya Theo Walcott kuwapa furaha ya muda
mfupi mashabiki wao kwa kufunga bao dakika 20.
Lakini, Robert Lewandowski aliisawazishia
Bayern Munich bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 55, huku beki Laurent
Koscielny wa Arselan akitolewa nje kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Nahodha wa Real Madrid, Sergio
Ramos, akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake bao dhidi ya Napoli.
|
Alvaro
Morata akishangilia bao la tatu alilofunga dhidi ya Napoli.
|
Katika mechi nyingine ya Klabu Bingwa Ulaya, Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos
aliisawazishia timu yake bao la kwanza
dakika ya 51 dhidi ya Napoli, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa San Paolo
nchini Italia.
Napoli, katika mechi ya kwanza iliyochezwa
jijini Madrid, Hispania ilipigwa mabao 3-1, ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika
ya 24, lililowekwa kimiani na Dries Mertens.
Lakini, Ramos aliisazishia timu yake
bao hilo kwa mpira wa kichwa, huku akisababisha la pili kwa mpira wa kichwa
uliogonga Mertens dakika ya 57.
Alvaro Morata aliyetokea kwenye
benchi aliifungia Real Madrid bao la tatu dakika ya 90 na kuiwezesha timu yake
kusonga mbele hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 6-2.
No comments