BASATA YAITAKA KAMATI YA MISS TANZANIA KUMKABIDHI MSHINDI GARI YAKE
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii
Ikiwa
imepita zaidi ya miezi minne tangu shindano la Miss Tanzania 2016
lifanyike huko jijini Mwanza na taji lake kuchukuliwa na mrembo Diana
Edward, bado mrembo huyo hajakabidhiwa zawadi yake ya gari na kiasi cha
pesa Shilingi milioni mbili.
hata
hivyo katika siku ya mwisho wa shindano hilo, mrembo Diana alionekana
akikabidhiwa gari aina ya Toyota IST, Ukumbini hapo kumbe ilikuwa
danganya toto kwa watu wote waliofika katika shindano hilo ili waweze
kuamini kuwa mrembo huyo kuwa kapewa gari.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura
akionekana kumkabidhi gari mrembo huyo siku muda mfupi baada ya
kutangazwa mshindi.
|
Diana
ambaye alikaa kwenye gari hiyo akiwa na furaha kubwa sana akimini kuwa
ndio mchuma wake wa kwenda nao nyumbani kwao lakini mpaka leo mrembo
huyo bado ni mtu wa kupanda daladala , Bajaj na Bodaboda.
Akizungumza
na Ripota wetu, afisa habari wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Agnes
Kimwanga amesema kuwa waliwaita kamati ya Miss Tanzania katika kikao cha
tahmini na wao kukiri kuwa hawajampatia zawadi zake zote mshindi huyo
pamoja na washiriki wengine wanne.
“mara
baada ya kujieleza katika kikao chetu cha Tathmini wakajitetea kuwa
watatoa zawadi hizo tarehe 30 Aprili mwaka huu kwa kumpa Miss Tanzania
2016 zawadi yake ya gari na kiasi chake cha pesa Milioni mbili ambacho
kimebaki” Amesema Agnes.
Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwa na washiriki wenzake siku aliyotwaa taji hilo.
|
Akithibitisha hilo, Afisa habari wa Miss Tanzania, Haiden Ricco alikiri kutomlipa mrembo huyo stahiki zake zote ikiwepo gari.
"Ni kweli mrembo wetu hajawalipwa na sio yeye peke yake, hata wale warembo wengine wanne hawajalipwa pia" alisema Ricco.
Amesema
kuwa fedha zilizobakia wanazodaiwa na warembo hao ni kiasi cha jumla ya
shilingi milioni nane hivyo zote watalipwa kuanzia mwezi huo wanne.
Rico
ametaja kuwa shindano lao kwa kutegmea wadhamini wamejipanga kuanzia
mwezi ujao kuanza kuwalipa warembo hao kadri watakavyokuwa wanapata
fedha kutoka kwa wadhamini na wadau wa shindano hilo.
No comments