Balozi aipa tano Azam FC, atoa mkono wa ushindi vs Mbabane
Balozi wa Tanzania nchini Afrika
Kusini, Richard Lupembe (mwenye suti nyeusi), akiwa na wachezaji wa Azam FC |
By Abducado Emmanuel on March 17,
2017
BALOZI wa Tanzania nchini Afrika
Kusini, Richard Lupembe, ameweka wazi kuwa Azam FC ni moja ya timu
zinazowatia moyo kama Watanzania wanoishi nje ya nchi, huku akiipa mkono wa
ushindi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows ya Afrika
Kusini.
Lupembe alitoa kauli hiyo wakati
alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini
Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika
utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa
10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
“Kwa kweli nimefarijika sana kwa
kuiona Azam FC tena kama nakumbuka mlikuja hapa mwaka jana, mlikuja hapa
kucheza (vs Bidvest) na nikawa mgeni rasmi na mkono wangu ukawa wa kheri
mkashinda, nawahakikishieni nitawashika tena mkono na ninauhakika mtashinda
tena,” alisema Lupembe wakati akizungumza na mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz
Alisema kuwa atakuwa pamoja na timu
hiyo kwa kipindi chote itakapokuwa jijini hapa hadi Jumamosi itakapoelekea
Swaziland huku akiitakia kila la kheri kuelekea mtanange huo unaosubiriwa na
mashabiki wengi wa timu hizo.
“Ndio tunafahamu kuwa kuna timu
kubwa za Simba na Yanga, lakini Azam FC inatia moyo kwa sisi watu ambao tulioko
nje nawatakia kila la kheri, mazoezi mema mimi nipo hapa kama balozi, na
nitahakikisha nitakuwa na nyie mpaka siku mtakapoenda kucheza mpira,” alisema,
Lupembe aliitembelea Azam FC jioni
wakati ikielekea kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo huo.
Mara mwisho Balozi huyo kuishika
mkono Azam FC iliichapa Bidvest Wits mabao 3-0 jijini Johannesburg katika
mchezo wa raundi kama hii, ambapo kutokana na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa
kwanza kwa sasa timu hiyo inahitaji ushindi wowote au sare ili iweze kusonga
mbele
Wachezaji wakifanya mazoezi |
Kocha akiwaelekeza jambo wachezaji wake |
No comments