ZANTEL, BAKWATA WAZINDUA HUDUMA YA MPYA YA “ZANTEL MADRASA JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi
wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo
ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo
pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji
wa mtandao wa Zantel watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga
simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo.
Mufti Mkuu wa
Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza mapema leo jijini Dar es
salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa
jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya
Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho
kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Zantel
watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe
mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo. (katikati) ni Mkurugenzi
Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa
Zantel Hamza Zuheri.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Aboubakar Zubeiry na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin wakionyesha
vipeperushi vya huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ kuashiria uzinduzi rasmi
wa huduma hiyo uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya
wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya
uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia
mtandao wa Zantel mahususi kwa waumini wa dini ya
Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho
kupitia simu za mkononi. (Katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Bw. Hamza Zuheri.
Mwandishi wa gazeti la The Citizen Alawi Masare (Kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit
Janin (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Zantel Rukia Iddi
Mtingwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo
ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini
hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi.
- Waumini wa dini ya Kiislamu sasa watajifunza masuala ya dini kupitia simu za mkononi
16 Februari 2017, Dar es Salaam-
Zantel kwa kushirikiana na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
imezindua huduma mpya inayojulikana kama ‘Zantel Madrasa’ ambayo
itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza kuhusu imani ya dini
hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu zao za mkononi.
Huduma hiyo itajumuisha mambo
mbalimbali kama vile Hadithi, Quran, Dua na huduma nyingine nyingi
kupitia ‘App’ kwenye simu ya smartphone ((IVR/SMS/Mobile App and Bakwata
News), ambapo pia mteja ataweza kupata taarifa kwa kupiga simu.
Akizungumza wakati wa sherehe ya
uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mkurugenzi
Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema, “Tunafuraha kuzindua huduma hii ya
‘Zantel Madrasa’ ambayo itawaunganisha waumini wa dini ya Kiiislamu
nchini na kuwawezesha kupata maarifa ya dini hiyo kwa urahisi zaidi.”
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa
BAKWATA, Mufti Abubakar Zuberi ambae alikua mgeni rasmi alisema, “Hii ni
huduma ya kipekee kwa jumuiya ya Waislamu na kila mtu anayependa
kujifunza kuhusu dini ya Kiislamu. Nawaomba Waislamu wenzangu kutumia
fursa hii mpya na mjiunge kwa wingi ili kujua mambo yanayopaswa kufanywa
katika Uislamu.”
“Ninaamini kwamba huduma hii mpya
itarahisha kazi kwetu viongozi wa Kiislamu kwa kuwa mafundisho mengi
yatakuwa yanapatikana kupitia Zantel Madrasa,” alisema.
Aliongeza kwamba BAKWATA itaisaidia Zantel kuitangaza huduma hiyo hapa nchini Tanzania hususan katika misikiti.
Zantel Madrasa ni huduma ya kwanza
kuzinduliwa kwenye mitandao ya simu nchini Tanzania ikilenga kutoa
mafundisho ya dini na kuwaunganisha watu kujifunza kuhusu dini nchini.
Huduma hii inatoa fursa kwa
Waislamu wote kujiunga na huduma hii kwa kupitia namba maalumu za
mtandao wa Zantel, hivyo kuwezesha watumiaji wa simu zaidi ya milioni 1
kupata mafunzo ya Madrasa kwa siku.
Watumiaji wa mtandao wa Zantel
ambao watapenda kuitumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma
ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo utakayopewa ili
kuunganishwa na kufurahia huduma hii.
No comments