Header Ads

ad

Breaking News

YANGA KAMA WAFALME UWANJA WA NDEGE DAR, WANACHAMA WAJITOKEZA KUWALAKI

Mwandishi Wetu
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa, Yanga, leo imetua uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kupokelewa kama wafalme wakitokea nchini Comoro.

 Yanga wakiwa Comoro walipepetana na Ngaya de Mde ya nchini humo na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1, hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo. Msimu uliopita Yanga ilifika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Furaha iliyokuwepo uwanjani hapo kwa mashabiki wao, iliwafanya wachezaji hao watulie kwanza, lakini baada ya hapo manahodha Nadiri Haroub 'Cannavaro' na Haruna Niyonzima, walikwenda kumwona mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa, Dar es Salaam. Manahodha hao waliongozana na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwassa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, manahodha hao walipata fursa ya kuonana na mwenyekiti wao na kubadilishan a naye mawazo, kabla ya kuungana na wenzao kambini.

Yanga wamesema kuwa, watajiandaa vizuri kwa ajili ya mechi yao ya marudiano dhidi ya Ngaya de Mde Februari 18, mwaka huu itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Mashabiki wa Yanga wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuipokea timu yao ambayo imewasili leo ikitokea Comoro ambako iliitwanga Ngaya kwa mabao 5-1 katika mechi ya kwanza ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.















No comments