Waziri SIMBACHAWENE ateta na Viongozi wa CWT Kuhusu Madai ya Walimu
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
George Simbachawene akisikiliza maelezo ya madai ya Walimu kutoka
kwa Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania
(CWT) Ezekiel Oluoch katika mkutano ulofanyika katika ofisi za TAMISEMI
kujadiliana juu ya madai ya Walimu leo mjini Dodoma.
Mkutano huo ulihusisha ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Tume ya utumishi ya Walimu (TSC), Wizara ya Fedha na Mipango, na Ofisi ya Rais Utumishi.
Mkutano huo ulihusisha ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Tume ya utumishi ya Walimu (TSC), Wizara ya Fedha na Mipango, na Ofisi ya Rais Utumishi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI)
George Simbachawene akiongea na wajumbe wa Chama Cha Walimu
Tanzania (CWT) katika mkutano uliofanyika katika ofisi za TAMISEMI
kujadiliana
juu ya madai ya Walimu leo Dodoma.
.................................
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amekutana na
viongozi wa chama cha Walimu nchini (CWT) na kuzungumza nao baada ya
kutangaza mgogoro na serikali ifikapo Machi Mosi, mwaka huu, iwapo
madeni ya walimu hayatashughulikiwa.
Kikao
hicho kimefanyika katika Ofisi za Tamisemi mjini Dodoma ambapo Waziri
Simbachawene aliwashukuru viongozi wa CWT pamoja na ofisi ya utumishi
kwa kuweza kukaa pamoja ili kuepusha mgogoro huo.
Simbachawene
alisema katika kikao hicho waliweza kujadiliana na walimu kuhusu madai
yao kutokana na taasisi hiyo kuwapo chini ya Tamisemi, hivyo lazima
wakae pamoja.
Alisema
anashukuru hatua ya viongozi wa CWT wakiongozwa na Rais Gratian Mkoba
na Katibu Mkuu Ezekiel Oluoch, kwa kukubali kukaa pamoja na serikali
kuhusu kunusuru mgogoro wanaotarajiwa kuutangaza na kwamba serikali
imeyapokea yote na kupata muda wa kuyajadili.
Alisema
kwa kawaida mahali popote, lazima kuwepo na madai ya mwajiri na
mwajiriwa, hivyo serikai imeyapokea madai ya walimu hao na kuyapitia
kisha kuyatolea maamuzi.
No comments