WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA WAJITOKEZA KUHAKIKIWA ZANZIBAR-WAILIIA SERIKALI IWAONGEZE PENSHENI
Mkaguzi
wa Ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Bara, Bw. Paison Mwamnyasi
(aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa wastaafu wanaolipwa pensheni
zao na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
waliofika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, eneo la
Vuga, kwa ajili ya uhakiki.
Zoezi
la uhakiki likiwa linaendelea katika ofisi za Wizara ya Fedha na
Mipango Zanzibar, kulia ni mstaafu Bw. Amir Apacho akifanyiwa uhakiki na
Mkaguzi Bi. Mary Mauki.
Mkaguzi
wa Ndani Mkuu Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe (kushoto) akimfanyia
uhakiki Bw. Abas Abdulan (kulia) pembeni yao ni baadhi ya wastaafu
wakisubiri kupata huduma ya kuhakikiwa, katika Ofisi za Wizara ya Fedha
na Mipango Zanzibar, zilizoko katika eneo la Vuga.
Mchambuzi
mwandamizi wa mifumo ya kompyuta Bi. Magreth Ambrosi Akipokea namba
kutoka kwa mstaafu (aliyeko dirishani) aliyopewa kwa ajili ya uhakiki.
Uhakiki wa Wastaafu unafanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha na
Mipango-Zanzibar, katika eneo la Vuga.
Baadhi
ya wastaafu ambao ni wagonjwa wakisubiri kupata huduma wakiwa
wametengewa sehemu maalumu kwa ajili ya kupata huduma hiyo ya uhakiki.
Mkaguzi
wa Ndani Mkuu Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe, akifanya mahojiano na
waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.
kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Bw. Paison Mwamnyasi.
Watumishi
wa Wizara ya Fedha na Mipango wakibadilishana mawazo kuhusu namna
uhakiki unavyoendelea. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa Ndani Bw. Paison
Mwamnyasi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Benny
Mwaipaja, Mkaguzi wa Ndani Bw. Nicholaus Jalane pamoja na Mkaguzi wa
Hesabu za Serikali Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar Bw. Abdulrahim
Mohamed
Afisa
Tehama wa Wizara ya Fedha na Mipango akimfanyia uhakiki Bw Uleja Edward
katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, zilizoko eneo la
Vuga visiwani humo.
Waziri
wa Biashara, Viwanda na Masoko-Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali,
alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar kwa
ajili ya kufanyiwa uhakiki. Aliyesimama mbele yake ni Mkaguzi wa Ndani
Bw. Nicholaus Jalane.
…………………………………………………………………….
Benny Mwaipaja, WFM, Zanzibar
MAMIA ya wastaafu wa Taasisi za
Muungano kutoka visiwa vya Pemba na Unguja-Zanzibar, wanaolipwa na
Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wamejitokeza kwa wingi kuhakikiwa huku wakiiomba Serikali iwaongezee
pensheni kutokana na wengi wao kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Wakizunguza katika Ofisi za
Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, iliyoko katika eneo la Vuga,
wastaafu hao wamepongeza hatua ya Serikali ya kuwahakiki ili kufahamu
hali zao na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwabaini watu wasio na sifa ya
kupata malipo hayo kutoka Serikalini
Wastaafu Bi Sauda Ramadhani
Mpambalyoto na Abuu Ali Hamisi, wameiomba Serikali iangalie namna ya
kuwaongezea pensheni wataafu ambao wengi wao ni wagonjwa hawajiwezi na
wengine wana afya njema, wanalima, lakini wanahitaji kuwezeshwa na
Serikali ili waweze kumudu maisha ambayo wamesema yamepanda.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
Msaidizi, Bw. Stanslaus Mpembe, amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango
inaendesha zoezi la kuhakiki wastaafu wanaolipwa pensheni na wizara
hiyo ili kuhuisha taarifa za wastaafu kwa lengo la kupata kanzidata
(database) iliyo ili kuiwezesha Serikali kuwalipa wastaafu wanaostahili.
Amesema kuwa wastaafu wanaolipwa
na Wizara hiyo ambao hawatahakikiwa wataondolewa kwenye orodha ya malipo
ya pensheni kwa kuwa watakuwa wamekosa sifa.
Aidha Bw. Mpembe amesisitiza
wastaafu hao kufika wenyewe na sio kutuma wawakilishi, wakiwa na nyaraka
zote muhimu zikiwemo barua ya tuzo la kustaafu, barua ya kustaafu au
kupunguzwa kazini, nakala ya hati ya malipo ya kiinua mgongo au mkupuo,
barua ya ajira ya kwanza, kitambulisho cha pensheni, barua ya
kuthibitishwa kazini, kadi ya benki na picha mbili ndogo zilizopigwa
hivi karibuni.
Amesema kuwa zoezi la uhakiki wa
wastaafu wanaolipwa na Hazina, litakamilika Mkoa wa Dar es salaam
kuanzia Machi 6 hadi 10, mwaka huu 2017
Zoezi hilo la uhakiki
linaloendelea Zanzibar, lilianza Oktoba 20, 2016 katika mkoa wa Pwani na
limeshafanyika katika mikoa 25 ya Tanzania Bara ambayo ni Mbeya,
Iringa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Katavi, Rukwa, Morogoro, Dodoma,
Singida, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara,
Shinyanga, Simiyu, Geita, Kigoma na Tabora, Lindi na Mtwara.
No comments