Wanahabari watakiwa kuacha kuamini kila kitu, wasome
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (wa pili kulia)
akimpongeza Meneja wa Redio Jamii Orkonerei FM, Baraka David Ole Maika
baada ya kuwasilisha risala ya mafunzo ya ufundi kwa Redio za Jamii
wakati maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam jana. Kulia
Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Fredrick Ntobi, Wa tatu kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishili wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Wanne kulia Mkurugenzi wa Taasisi
ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr.
Edephonce Nfuka na Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa
Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper Kwigize.
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye
akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo
akisheheresha kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya radio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues akitoa
neno la ukaribisho liliombatana na ujumbe maalum kwenye sherehe za
maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Makamu
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper
Kwigize akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi Waziri Nape Nnauye (hayupo
pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani,
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye
akiteta jambo na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini
Zulmira Rodrigues (katikati) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya
redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu
Huria (OUT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya
Elimu na Menejementi ya Teknolojia wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr.
Edephonce Nfuka
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye
akimpongeza Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA)
Prosper Kwigize kwa hotuba nzuri wakati wa sherehe za maadhimisho ya
siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo
Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia wa Chuo Kikuu Huria
(OUT), Dr. Edephonce Nfuka na kulia ni Mkurugenzi wa Utangazaji wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi.
Mkurugenzi
wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi
akizungumza kuhusu taratibu na sheria za utoaji leseni kwa redio za
jamii nchini wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dk. Ayoub Rioba akifafanua
jambo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Meneja
wa Redio Jamii Orkonerei FM, Baraka David Ole Maika akitoa neno la
shukrani wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Washiriki
kutoka redio za jamii nchini na waandishi wa habari waliohudhuria
sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika
ukumbi wa Cho Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi
akiwasilisha mada kuhusu upashanaji wa vyombo vya habari na sheria
wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyoratibiwa
na UNESCO na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria
(OUT) jijini Dar es Salaam.
Mshauri
wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP)
Tanzania, Rogers Dhliwayo akizungumza kuhusu malengo ya maendeleo
endelevu (SDGs) na namna radio inavyowezesha hamasa ya utekelezaji wake
kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyoratibiwa na
UNESCO na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT)
jijini Dar es Salaam.
Meza
kuu kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye
(katikati) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa redio za jamii
nchini wakati sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape
Nnauye(katikati) na meza kuu katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi
ya COMNETA wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape
Nnauye(katikati) na meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Umoja wa Mataifa kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Maafisa
wa UNESCO Dar Luiana Temba (kushoto) na Rose Mwalongo Mataifa
wakifurahi jambo kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
SERIKALI
imewataka wanahabari kusoma sheria, taratibu na kanuni zinaogusa tasnia
yao ili iweze kuendelea na kuachana na kuamini kila kitu wanachoambiwa
na mtu mmoja.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.
Nape Nnauye wakati akizungumza katika siku ya radio duniani, hafla
iliyofanyika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.
"Watu
someni sheria, taratibu na kanuni kwa kina ili kujua na kuzielewa,
mkielewa kama kuna sheria inakwaza ukuaji wa sekta ya habari tuseme
tukae chini.. " alisema Waziri Nape akijibu hoja kuhusu sheria za habari
zilizopo ambazo zinadaiwa kukwaza uhuru wa ukusanyaji wa habari.
Ilielezwa
katika hafla hiyo kuwa sheria za sasa ya takwimu na habari zinakwaza
uhuru wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Katika
hoja hiyo Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA)
Prosper Kwigize katika hotuba yake kwa Serikali, alisema kwamba redio
hizo zinachangamoto nyingi katika utendaji wake ikiwamo sheria
zilizopo,watoa habari wasioeleweka na wanazuia upatikanaji wa habari.
Nape
alisema kwamba sheria si msaafu na kwa kuwa asilimia 80 za habari
zinazalishwa na serikali, waandishi wanahaki ya kupata habari hizo na
kama kuna kikwazo ni lazima kitafutiwe suluhu.
"Tukae
tushindane kwa hoja tukubaliane na kuhakikisha kwamba tunarekebisha..
Bunge kazi yake ni kutunga na kufuta sheria" alisema Nape ambaye alisema
kwamba sheria ya sasa imetoa nguvu kwa watoa habari na kwamba si kila
habari iliyopo serikalini ni classified.
Alisema
pia ili kufanikisha upatikanaji wa habari maofisa habari wamepewa
maagizo ya kushiriki vikao ili waweze kutoa taarifa bila woga na kwa
ujasiri mkubwa.
Alisema
ni kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kukua kwa tasnia
ya habari na itaendelea kupigania hilo kwa kuwa inatambua umuhimu wa
vyombo vya habari.
Pamoja
na kuweka mazingira mazuri amewataka wanaoendesha redio za jamii
kutafuta namna ya kujiunga na taarifa za kitaifa (habari) ili wananchi
wasitengwe na matukio ya maeneo mengine.
Alisema kwa kuwa sehemu kubwa ya redio hizo ziko pembezoni ni vyema nguvu yake ikatumika pia kuhabarisha matukio ya kitaifa.
Akizungumzia
dawa za kulevya, Waziri Nape alitaka wanahabari kuwa na uzalendo na
kushiriki katika vita hiyo kwa kutumia vyombo vyao vyote.
Alisema
ni vyema wananchi na wanahabari wakatambua kwamba vita hiyo ni yetu
sote na kwamba wanahabari wanauwezo wa kuunganisha wananchi katika
kushinda hiyo vita ambayo ni kubwa.
Akizungumzia
redio alitaka watu wanaotumia vyombo hivyo kuangalia namna ya kutoachwa
nyuma wakati huu wa mabadiliko makubwa ya teknolojia na sayansi ambapo
matumizi ya mtandao ya utoaji wa habari papo hapo unaendelea.
Aliwataka
watu kuzungumza nafasi ya radio katika kuleta maendeleo huku
wakiangalia changamoto zinazoletwa na teknolojia ya habari.
Sherehe
hizo ambazo ziliambatanishwa na midahalo kuhusu upashanaji wa vyombo
vya habari na sheria iliwasilishwa na Mkurugenzi wa utangazaji wa TCRA
Ntobi na pia watendaji wa UNDP kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na
namna radio inavyowezesha hamasa ya utekelezaji iliratibiwa na UNESCO.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues alisema
akimkaribisha Waziri Nape kwamba washiriki katika sekta ya utangazaji
wanatakiwa kuwa pamoja ili kukuza upashanaji wa habari katika maeneo ya
pembezoni.
Alishauri kuwepo na kuaminiana ili kufanikisha malengo ya kuleta maendeleo kwa kupeana nafasi na kushirikishana.
Alitaka watanzania kutumia nguvu ya radio kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kitaifa na kuleta maendeleo yanayotakiwa.
Kukiwa
na vituo vya radio 44,000 duniani Mwakilishi huyo wa UNESCO alisema
kwamba radio bado ina maslahi makubwa kwa wananchi kutokana na kutoa
sauti kwa wakazi ili kukabiliana na changamoto zilizopo.
No comments