TPDC WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA
Wanahabari
mkoa wa Iringa walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa
katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa
tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha
iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka
mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa.
Wanahabari
mkoa wa Njombe walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa
katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa
tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha
iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka
mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa
Wanahabari
mkoa wa Ruvuma walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa
katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa
tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha
iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka
mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa
Meneja
mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria
Mselemu (TPDC) akitoa neno wakati wa utangulizi wa warsha hiyo kwa
waandishi wa habari wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amelipongeza Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa
waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha, Iringa,Ruvuma na Njombe
ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ambayo
yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja mwaka huu(21 / 02
/2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.
“Ingawa
mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la
Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari katika kupata uelewa mpana
wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi ili waweze kuhabarisha na kuelimisha
watanzania kwa ujumla ili watambue shughuli za shirika na faida zake
haswa katika uchumi wa nchi”, alieleza Mkuu wa Wilaya.
Aidha
Mh Kasesela amewaomba Waandishi wa Habari kuwa wazelendo katika
kuisaidia Serikali kutekeleza miradi mbalimbali yenye maslahi mapana
katika maendeleo ya nchi yetu. ‘’Waandishi Wahabari mnapaswa kuisaidia
Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija kwa uchumi
wa Taifa, mfano katika vita ya kiuchumi ya kugombania mradi wa bomba la
mafuta ghafi kutoka Uganda kati ya Tanzania na Kenya, wenzetu Kenya
walijitahidi kuandika habari zenye kutoa wasifu wa nchi yao ili
kuisaidia kupata mradi huo, hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya kazi
kiuzalendo.”
Aliongeza
kuwa leo hii mmeweza kuifahamu TPDC sasa mnapaswa kuwaeleza wananchi
miradi inayofanywa na Shirirka hili na manufaa yake katika uchumi wa
Taifa, mwende mkatafiti namna mradi wa bomba la mafuta utakavyonufaisha
wananchi wanaoishi kando ya njia ya bomba hilo, vilevile namna bomba
hilo litakavyosaidia kukuza uchumi wa nchi, hivi ndivyo tunavyoweza
kujenga nchi yetu kupitia taaluma ya uandishi wa habari.
Kasesela
alisisitiza kuwa ili tujenge Taifa imara ni vyema tuandike habari kwa
weledi, uzalendo huku tukiondoa tofauti zetu za kiitikadi ziwe za
kikabila, kisiasa au kidini kwa namna hii tutaweza kuandika habari zenye
kujenga nchi yetu na si vinginevyo.
Alisisitiza
vile vile juu ya utoaji taarifa mapema pale mtu anapoona kuna hujuma au
uharibifu wa aina yoyote katika miundombinu hii, akiongea katika warsha
hiyo alisema “miundombinu hii ya gesi na mafuta ni mali ya watanzania
hivyo kuilinda ni jukumu letu sote kama wazalendo wa nchii hii”.
Akiongea
wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Afisa mahusiano wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu alisema warsha hii
inalenga kuendelea kuwajengea uwezo zaidi waandishi wetu wa habari
kuweza kuripoti kwa umahiri na ustadi habari za mafuta na gesi.
Mselemu
aliwashukuru waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuupasha habari umma
na kuwaasa kwamba kalamu yao ina nguvu hivyo ni vyema ikaendelea
kutumika kujenga uchumi wa Taifa kwa kutoa taarifa sahihi kila
wakati.Katika taarifa yake Faustin Kayombo kutoka mkondo wa juu (TPDC)
alisisitiza juu ya matarajio yasiyo halisia yaliyopo miongoni mwa
wanajamii na kuwaomba waandishi wa habari kusaidia kuwaeleza wananchi
juu ya uhalisia wa sekta.
Kayombo
alisema kwamba uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ni wa gharama
kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali huchukua
muda mrefu kuonekana.
Akitolea
mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG),
Kayombo alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya
mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa
mauzo.
Hata hivyo Kayombo alisisitiza juu ya ushiriki wa wazawa katika sekta hii hususan katika kutoa huduma na kuuza bidhaa.
Naye
mwanasheria wa TPDC Barnabas Mwashambwa alisema sheria mpya ya petroli
ya mwaka 2015 inawataka wawekezaji wote kutumia bidhaa zinazozalishwa
hapa nchini na kama ikitokea bidhaa hizo hazipo nchini basi kampuni
iingie ubia na kampuni ya kizawa ili kuweza kutoa huduma inayohitajika.
Sheria
imeeleza kwamba ubia huo lazima umpe mzawa ushiriki usiopunguza
asilimia 25%, hii ni fursa kwa wazawa na ni vyema ikachangamkiwa. Hata
hivyo Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa frank leornad
ameliomba Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutenga muda
wa kutosha zaidi katika uelimishaji ili walengwa waweze kuelewa vyema
sekta, ombi ambalo liliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya.
Katika
mafunzo hayo waandishi wa habari walipata fursa ya kujifunza kuhusu
maendeleo ya Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Gesi Asilia na
Faida Zake, Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda
hadi Tanga na Usambazaji wa Gesi Asilia Majumbani, Viwandani na kwenye
Vituo vya Kujaza Magari.
TPDC
imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza
uelewa zaidi katika sekta hii mpya na changa ya mafuta na gesi hapa
nchini.
No comments