TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA LAREJEA KWA KISHINDO
Baada
ya ukimya wa mwaka mmoja bila tamasha la muziki pendwa la Zanzibar,
Tamasha la Sauti za Busara 2017 limerejea kwa kishido ambapo band 40 na
wasanii zaidi ya 400 walitumbuiza kwenye majukwaa matatu tofauti kwa
siku nne mfululizo. Tamasha linalotumbuiza asilimia 100 live muziki wa
Africa ulijumuisha nyimbo za kitamaduni kutoka kwa wasanii chipukizi na
wasanii pendwa kama Bob Maghrib (Morocco), Mcharuko Band (Zanzibar), Ze
Spirits Band (Tanzania), H_art the Band (Kenya), Madilisto Band
(Malawi), Pat Thomas & Kwashibu Area Band (Ghana), Karyna Gomes
(Guinea-Bissau) na wengine wengi.
Wahudhuriaji wa tamasha elfu
sita kutoka mataifa mbalimbali walihudhuria Ngome Kongwe, Zanzibar, hali
ilikua ya kuburudisha. Jukwaa la Forodhani lilikua maarufu kwa vijana
na familia za Zanzibar zilizokusanyika kufurahia wasanii wakitumbuiza
huku wakishudia jua lianazama.
Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi wa
Tamasha muda mfupi baada ya tamasha alisema “Kupitia lugha ya kuziki
Sauti za Busara imenonesha dunia kuwa Africa imejawa na matumaini,
furaha na utajiri wa kutosha kwa upande wa utamaduni. Kwa wiki moja
aelfu ya watu wa Zanzibar na sehemu mbalimbali duniani wameshuhudia
nguvu ya muziki inavyokuza amani, urafiki na umoja. Ninawashuluru
wasanii wote na wafanyakazi wote wa Busara, watu wa Zanzibar, wadhamini,
vyombo vya habari, na kila mmoja aliyehudhuria na kuchangia mafanikio
haya,”.
Wahudhuriaji wengi wamesema
tamasha la mwaka huu lilikua zuri kuliko mengine lililosheheni ratina
nzuri yenye muziki wa kiwango cha juu kwa upande wa sauti na taa. Pia
utaratibu wa kila kitu ulipangwa vizuri na mambo yote yalifanyika bila
tatizo lolote ndani ya muda uliopagwa.
Mwaka huu, Busara Promotions
wameshirikiana na Taasisi ya Emerson Zanzibar na kuzindua rasmi tuzo ya
kwanza ya muziki ya Emerson iliyompa tuzo msanii bora wa Zaznibar
kutoka kundi lililotumbuiza tamasha la Sauti za Busara 2017. Tuzo
imeenda kwa Gora Mohammed Gora, anayepiga Ganun kwenye band ya Matona’s
G Clef. Mohammed aipata dola za Marekani 1,000, kombe, cheti na sherehe
iliyoandaliwa na Emerson Spice Hotel.
Eneo lote la Stone Town, mitaa ilijazwa na sauti za muziki pamoja na Busara Xtra
ratiba iliyoandaliwa kufikisha muziki kwa watu. Kina mama kutoka chuo
cha Madrassat Michenzani waliimba “Dufu,” ngoma ya asili ambayo mara
nyingi huimbwa na kupigwa na wamaume ila kudi hili la wanawake walianza
mud mrefu na walishangaza umati wa Busara kwa uimbaji wao.
Mada za Movers & Shakers
zilielezea changamoto za wanawake na muziki kwenye mada maalumu
iliyoshirikisha wasanii mbalimbali. Mariam Hamdani, Mkurugenzi wa kundi
la Tausi Women’s Taarab, alisema ndoa sababu kubwa inayowakwamisha
wanawake wasifanikiwe kwenye kazi ya muziki. “Wanawake kwenye kudi letu,
hupoteza vipaji vizuri kwa sababu ya ndoa baada ya waume zao kuwakataza
kuendelea na kazi hiyo baada ya kuwaoa,” amesema Mariam Hamdani.
Wakati hadhira ikihitaji burudani zaidi, Sauti za Busara imepangwa kurejea mwaka ujao Februari 8-11, 2018.
Sauti za Busara 2017
imedhaminiwa na Ubalozi wa Norway, Swiss Agency for Development
Cooperation (SDC), ZANTEL, SMZ, Africalia, Ubalozi wa Ujerumani,
Zanlink, Memories of Zanzibar, Ethiopian Airlines, Mozeti, Coastal
Aviation, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Music in Africa, Chuchu FM
Radio, Tifu TV na Zanzibar Media Corporation.
No comments