TAASISI YA MOYO KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA BLK YA NCHINI INDIA WATOA HUDUMA YA MATIBABU YA MOYO BILA YA KUFUNGUA KIFUA KWA WAGONJWA 16
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK
ya nchini India wakimwekea mgonjwa kifaa kitakachosaidia moyo kupata
umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK
hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK
ya nchini India wakimwekea mgonjwa betri ambalo litatumiwa na kifaa
kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI
kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab
wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Daktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuhudumia Monica Mahenge ambaye
amelazwa katika Taasisi hiyo baada ya kufanyiwa matibabu ya moyo kupitia
mishipa ya damu bila
kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab .
Monica ni mmoja kati ya wagonjwa 16 ambao JKCI kwa kushirikiana na
wataalamu kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India walitoa huduma za
matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve), balloon mitral valve procedure (Valvuloplasty), kuzibua mishipa ya damu ya moyo, kufunga kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme (Pacemaker) na kuangalia utendaji kazi wa Moyo.
Madaktari bingwa wa Moyo, Wauguzi, Technologists, wataalam wa dawa za usingizi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kumpatia mgonjwa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve) bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab .
Kazi ya kutoa huduma ya matibabu ya Moyo kwa mgonjwa kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab ikiendelea.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
No comments