TAARIFA KUTOKA JWTZ:UTAPELI AJIRA JWTZ
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 20 Februari, 2017.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa na taarifa za kutapeliwa wananchi kuhusu ajira za JWTZ.
Hivi
karibuni kumezuka kundi la watu wanao jiita mawakala wa kutafuta vijana
wa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na mara nyingi
hutumia majina ya viongozi wa JWTZ kutapeli, huwataka wananchi hao
kuwapa fedha ili kuweza kuwapatia nafasi hizo.
JWTZ
linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa nafasi za ajira Jeshini
hutangazwa kwa kufuata taratibu za ajira ambapo JKT imepewa mamlaka ya
kuwachukuwa vijana kutoka uraiani kwa kutoa matangazo ya wito wa vijana
wa kujitolea ambapo matangazo hayo hutolewa hadi ngazi ya wilaya, vijana
hao hutakiwa kuwa na nyaraka mbali mbali zikiwemo za elimu, uraia na nyaraka nyingine kama hizo ili kukidhi vigezo vya kupatiwa mafunzo ya kijeshi.
Baada
ya kumaliza mafunzo hayo wahitimu hubaki JKT kwa muda wakisubiri vyombo
vya ulinzi na usalama likiwemo JWTZ kutoa ajira kulingana na hitajio la
vyombo hivyo. Wananchi wanatakiwa kufuata taratibu hizo ili kuepuka
udanganyifu unaoweza kusababisha kutapeliwa fedha zao. Jeshi
halitahusika na madai yoyote yatakayotokana na udanganyifu huo.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
No comments