Header Ads

ad

Breaking News

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

msangii
TAREHE  06.02.2017 MAJIRA YA SAA 01:00HRS USIKU, KATIKA CHUO CHA UTAFITI WA SAMAKI NA UVUVI KILICHOPO MTAA WA BUTIMBA  WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WATANO WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA ZA MAPANGA, VIPANDE CHA NONDO NA  WAKIWA WAMEVALIA MAKOTI MAREFU HUKU WAKIWA NA FUNGUO BANDIA WALIVAMIA OFISI ZA CHUO TAJWA HAPO JUU NA KUJARIBU KUVUNJA OFISI  KWA LENGO LA KUPORA  FEDHA, SAMAKI NA  VITU MBALIMBALI VILIVYOMO NDANI, POLISI WALIWAPA AMRI YA KUKAA CHINI YA ULINZI LAKINI WALIKAIDI NA KUANZA KUKURUPUKA KUKIMBIA, NDIPO ASKARI WALIFYATUA RISASI KADHAA HEWANI HUKU WAKIWAAMURU KUJISALIMISHA LAKINI WALIKAIDI AMRI HIYO, ASKARI  WALIWAFYATULIA RISASI ZA MIGUUNI ZILIZOWALENGA MAJAMBAZI  WAWILI NA KUFANIKIWA  KUWAKAMATA  AMBAO NI 1. RASHIDI SPAKI MIAKA 37, MUHA NA MKAZI WA MKOLANI NA 2. ADAM MBALAMWEZI @ SAIDI MIAKA 38, MNYAMWEZI NA MKAZI WA IGOGO, HUKU MAJAMBAZI WENGINE WATATU WAKIFANIKIWA KUTOROKA.
ASKARI WALIWACHUKUA MAJAMBAZI HAO WALIOJERUHIWA KWA RISASI NA KUWAKIMBIZA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KWA AJILI YA MATIBABU ILI BAADAE WAKIPONA WAWEZE KUHOJIWA, WATUHUMIWA WALIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI ZAO ZILIKUWA ZIKIENDELEA VIZURI LAKINI ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA 5:00HRS ALFAJIRI YA TAREHE TAJWA HAPO JUU, MTUHUMIWA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA RASHIDI SPAKI ALIYEJERUHIWA KWA RISASI  KWENYE PAJA/NYONGA JUU KUSHOTO ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, AIDHA MWENZAKE AITWAYE ADAM MBALAMWEZI ALIYEPATA JERAHA KWENYE MGUU WA KUSHOTO ALIKUWA AKIENDELEA VIZURI NA TAYARI AMERUHUSIWA HOSPITALI YUPO POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI.
AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA WATU MAJAMBAZI AMBAO WAMEPANGA KUVAMIA OFISI TAJWA HAPO JUU WAKIWA NA SILAHA NDIPO UFUATILIAJI WA HARAKA JUU YA TAARIFA HIZO ULIFANYIKA, ASKARI WALIFIKA MAPEMA ENEO LA TUKIO NA KUWEKA MTEGO WA KUWAKATA MAJAMBAIZI HAO, GHAFLA MAJAMBAZI WATANO WALIFIKA ENEO LA TUKIO WAKIWA WAMEVALIA MAKOTI MAREFU WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUVUNJA OFISI NA KUPORA. POLISI WALIWAZINGIRA MAJAMBAZI HAO NA KUWAPA AMRI YA KUKAA CHINI YA ULINZI LAKINI WALIKAIDI NA KUKURUPUKA NA KUANZA KUKIMBIA NDIPO  ASKARI WALIFYATUA RISASI KADHAA HEWANI HUKU WAKIWAAMURU MAJAMBAZI HAO KUJISALIMISHA LAKINI WALIENDELEA KUKAIDI AMRI HIYO, NDIPO ASKARI WALIWAFYATULIA RISASI ZA MIGUUNI  ZILIZOWALENGA  MAJAMBAZI WAWILI TAJWA HAPO JUU, HUKU MAJAMBAZI WENGINE WATATU WAKIFANIKIWA KUTOROKA.
KATIKA TUKIO HILO ASKARI WALIWEZA KUKAMATA MAPANGA MAWILI, NONDO, TUPA NA FUNGUO BANDIA AMBAZO ZILIKUTWA KWENYE SURUALI ALIYOVAA MAREHEMU BAADA YA KUFANYIWA UPEKUZI. WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WALIPOHOJIWA WALIKIRI TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA MATUKIO KADHAA YA UHALIFU YALIYOTOKEA HAPA JIJINI MWANZA, AIDHA WALIKIRI TUHUMA ZA SKUHUSIKA KWENYE TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA LILILOTOKEA KATIKA GHALA LA KIWANDA CHA VICK FISH KILICHOPO IGOGO WILAYA YA NYAMAGANA AMBAPO MAJAMBAZI HAO WALIVUNJA NA KUPORA MABONDO YA SAMAKI YENYE THAMANI YA TSH 150,449,400/=, AMBAPO ILIFUNGULIWA KESI YENYE KUMBU NAMBA MWS/IR/439/2016.
AIDHA WALIKIRI PIA TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA MARA YA PILI KWENYE KIWANDA HICHOHICHO CHA VICK FISH KILICHOPO IGOGO AMBAPO WALIVUNJA USIKU LAKINI HAWAKUFANIKIWA KUPORA KITU CHOCHOTE KWANI WAKATI WAKIWA KWENYE JITIHADA ZA KUTOA MABONDO YA SAMAKI POLISI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA MAJAMBAZI HAO WALIKIMBIA, AMBAPO ILIFUNGULIWA KESI YENYE KUMBU NAMBA MWS/1R/5807/2016, YA KOSA YA KUVUNJA GHALA USIKU KWA NIA YA KUIBA.
POLISI WANAENDELEA NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA AMBAYE ANAENDELEA KUSHIKILIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, UPELELEZI NA MISAKO JUU YA WATUHUMIWA WENGINE WATATU AMBAO WALIFANIKIWA KUTOROKA UNAENDELEA ILI WAKAMATWE PIA WATOE SILAHA AMBAYO  WANAYO, MWILI WA MAREHEMU UPO HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WAHALIFU NA UHALIFU MAPEMA, ILI KUWEZA KUZUIA LAKINI PIA ILI WAWEZWE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA. AIDHA ANAWASIHI VIJANA KUFANYA KAZI ZILIZO HALALI ILI WAJIEPUSHE NA MATATIZO AMBAYO YANAWEZA KUGHARIMU MAISHA YAO.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments