Serikali kufanikisha Soka kushiriki Olimpiki Tokyo 2020
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa soka leo
Jijini Dar es Salaam kuhusu namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza
kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao
cha Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa soka leo
Jijini Dar es Salaam kuhusu namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza
kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao
cha Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akieleza jambo
kwa wadau wa Soka (hawapo pichani) kuhusu namna gani timu ya Soka ya
Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo
2020 leo Jijini Dar es Salaam katika kikao cha Wadau Tuzungumze
kilichoandaliwa na Wizara.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Omary
Singo akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Wizara katika kufanikisha timu
ya soka ya Tanzania kushiriki Olimpiki Tokyo 2020 leo Jijini Dar es
Salaam katika kikao cha Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara.
Msemaji wa Shirikisho la Soka
nchini (TFF) Bw. Alfred Lucas akichanhia mada wakati wa kikao cha
kujadili namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na
kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao cha Wadau
Tuzungumze kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Usuluhishi na
Nidhamu kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bibi: Zainab Mbiro akitoa
maoni yake kuhusu namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki
na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao cha Wadau
Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wadau wa soka nchini baada ya kumaliza kikao cha kujadili
namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda
michezo ya Olimpiki Tokyo 2020 kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………….
Na Lorietha Laurence.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa wadau wa michezo
nchini kushirikiana na Serikali kwa kupeleka michezo mbalimbali ikiwemo
soka kwenye mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa kufanyika mjini Tokyo
Japan mwaka 2020 ili kupata nafasi ya kushinda.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es
Salaam alipokutana na wadau wa soka katika muendelezo wa kipindi chake
cha “Wadau Tuzungumze” lengo ikiwa ni kujadili namna ambavyo timu ya
mpira wa miguu itakavyoweza kushiriki katika mashindano hayo ya
Kimataifa.
Ameongeza kwa kusema kuwa
ushiriki wa timu za mpira wa miguu kwenye mashindano ya Olimpiki ni
muhimu katika kukuza na kuendeleza soka huku akiwataka wadau hao
kupeleka michezo mingi zaidi ili kupata nafasi ya kushinda medali
mbalimbali.
“ Lengo letu ni kupata ushindi
hivyo kwa kupeleka michezo mingi katika mashindano haya ya Olimpiki
tunajitengenezea nafasi nzuri ya kurudi na ushindi na kuondokana na
dhana ya kuwa washiriki ” alisema Mhe.Nape
Aidha aliwataka watanzania
kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha tunapata ushindi kwa kuwapa
moyo wachezaji wetu ikiwemo uhamasishaji kupitia wadau mbalimbali
wakiwemo wasanii wa muziki wa kisasa.
“Ushindi ni wetu sote hivyo ni
wajibu wetu kuweka juhudi za dhati katika kuhamasisha wachezaji kwa
kuwapa moyo ili waweze kurudi na ushindi na tayari nimeunda timu ya watu
kumi kwa ajili ya kuhamasisha ushiriki wa Serengeti Boys katika
mashindano ya AFCON Gabon” alisema Waziri Nape.
kamati hiyo itakayoongozwa na
Charles Hillary itakuwa na wajumbe wengine ambao ni Selestine
Mwesigwa,Beatrice Singano,Hassan Abbas, Ruge Mutahaba,Hoyce Temu,Eric
Shigongo, Maulid Kitenge, Naseeb Abdul(Diamond) na Ally Kiba.
No comments