Rais Museveni Awakaribisha Watanzania Kuwekeza Nchini Uganda
Na. Immaculate Makilika na Lilian Lundo- MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni ametoa wito wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini Uganda.
Rais
Museveni ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea viwanda vya Kampuni
ya Bakhresa vinavyozalisha Unga na Juisi vya Buguruni na Vingunguti
jijini Dar es Salaam.
“Nawakaribisha
wafanyabiashara wa Kitanzania kuja nchini Uganda kuwekeza kwani kufanya
hivyo kutasaidia kuzalisha bidhaa, upatikanaji wa soko pamoja na ajira”
alisema Rais Museveni.
Kauli
hiyo ya Rais Museveni imetokana na mafanikio yanayotokana na Mwekezaji
wa Kitanzania Said Salim Bakhresa aliyewekeza nchini Uganda ambapo
anamiliki Kiwanda cha kusanga ngano nchini humo.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni za Bakhresa Hussin Sufiani
amesema kwamba Kampuni hiyo iko mbioni kuongeza uzalishaji wa unga wa
ngano kutoka tani 1,100 hadi kufikia tani 2,000 kwa siku nchini Uganda.
Aidha,
amesema kutokana na uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Uganda jumla ya
Waganda 650 wamenufaika na ajira mbalimbali ambazo zinasaidia kuwapatia
kipato.
Kwa
upande wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwaijage amesema kuwa Uganda na Tanzania zimeingia makubaliano ya
ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya viwanda.
Amesisitiza
Watanzania wanaweza kwenda kuwekeza nchini Uganda kwa vile nchi hiyo
wanalima tani milioni 4 za mahindi lakini wana uwezo wa kutumia tani
milioni moja pekee, hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania
kwenda kuwekeza nchini humo.
“Tunawahamasisha
wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania kuwekeza katika nchi zao ili
kuzalisha , bidhaa na ajira za kutosha kwa wananchi” alisema Waziri
Mwijage.
Waziri
Mwijage alitoa Wito kwa Watanzania kushiriki katika uchumi wa viwanda
kwa kufanya uzalishaji wa bidhaa zinazotumika viwanda mfanio kwa kulima
matunda au mbogamboga.
Rais
Yoweri Museveni aliwasili nchini jana kwa ziara ya kiserikali ya siku
mbili ambapo akiwa nchini alifanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na
kutembelea Viwanda vya Said Salim Bakhresa vya Tazara na Vingunguti.
No comments