Header Ads

ad

Breaking News

Mkurugenzi Mkuu TBL Group asema wataalamu ni nguzo muhimu kufanikisha biashara endelevu

tib1
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Masoko Kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin (kulia) akifafanua jambo kwa  wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaosoma  Programu ya utawala wa Biashara ya Chuo cha Swedish Institute wakati walipofanya ziara ya mafunzo  katika kiwanda cha bia cha Ilala jijini Dar es salaam
tib2
Meneja wa kiwanda cha TBL Ilala akiongea na wanafunzi kuhusu mifumo ya uendehaji bora wa viwanda
tib3
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Masoko Kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin akibadilishana mawazo na baadhi ya wanafunzi na wakufunzi kutoka Swedish Institute
tib4
Mmoja wa wanafunzi anayesoma katika Programu ya Biashara na Utawala ya  Swedish Institute  Ng’winula Kingamkono (kushoto) akiuliza swali kwa watendaji wa TBL Group
tib5
Mtaalamu wa upishi wa bia kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam, Calven Naiman,akiwaeleza wanafunzi hao jinsi upishi wa bia  unavyofanyika
tib6
Baadhi ya wanafunzi  kutoka taasisi ya Swedish Institute wakibadilishana mawazo  wakazi wa ziara hiyo ya mafunzo
tib7
Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL Group  Ilala jijini Dar es Salaam, Calvin Martin,akiwaongoza wanafunzi kutembelea maeneo ya kiwanda
tib8
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (kushoto)  akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wanafunzi  ,Eric Muthomi,kwa niaba ya wenzake 
……………………………………………………………………..
Asema mafanikio ya kampuni yake yanaletwa na wafanyakazi wenyewe
 
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto jarrin,amesema uanzishwaji wa biashara na uwekezaji unaofanywa kwenye nchi za Afrika unatoa mchango wa kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira hivyo kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha kunakuwepo wataalamu wa kubuni na kuendesha mifumo ya kisasa ya biashara ili biashara hizo zizidi kukua na kuwa endelevu.
 
Roberto aliyasema  hayo mwishoni mwa wiki wakati akiongea na wafanyakazi  kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika ambao wanahudhuria mafunzo  ya ukuzaji wa biashara endelevu  chini ya mpango ujulikanao kama Swedish Institute Management Programme unaolenga kuwajengea uwezo wa biashara na utawala vijana wasomi kutoka barani Afrika walipotembelea kiwanda cha TBL cha Ilala jijini Dar es Salaam.
 
Alisema biashara yoyote inayoendeshwa kwa kufuata misingi ya kitaalamu ni lazima ipate mafanikio na kuwa endelevu “Biashara ikiendeshwa kwa misingi ya kitaalamu inakua kwa haraka na kuchangua kukuza uchumi wa nchi,kuongeza wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja,kuchangia pato kubwa kwa serikali kwa njia ya kulipa kodi na kunufaisha jamii kwa namna mbalimbali”.
 
Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa TBL Group kupitia viwanda  vyake vilivyopo kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa kiasi kikubwa imekuwa ikizingatia kuendesha shughuli zake kwa kufuata misingi bora ya uendeshaji biashara ambayo kwa kiasi kikubwa imewezesha kampuni kupata mafanikio mengi na kuwa kioo cha uwekezaji bora ambapo watu kutoka sehemu kadhaa wamekuwa wakitembelea viwanda vyake kwa ajili ya kujifunza mifumo ya uzalishaji bora wenye tija na ufanisi.
 
Kampuni ya TBL Group imekuwa ikifanya vizuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia pato la taifa kwa njia ya kulipa kodi,utunzaji wa mazingira,kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kupitia mtandao wa biashara zake,kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo inaoshirikiana nao,kuendesha kampeni ya unywaji wa kistaarabu kwenye jamii,kuwezesha wakulima ambao wanaiuzia malighafi na imekuwa kinara wa kutekeleza kanuni bora za ajira ambapo imekuwa ikishikia rekodi ya kupata tuzo ya Mwajiri bora inayotolewa na Chama cha Waajiri nchini (ATE)”.
 
Roberto alisema kuwa mafanikio haya hayatokani na kufuata mifumo bora ya uzalishaji pekee bali ni kuwa na wafanyakazi wenye vipaji vikubwa na taaluma mbalimbali ambao wanafanya kazi kwa kujituma wakati huohuo kampuni ikiwa inawapatia motisha na mafunzo ya  kwa mara ili kuhakikisha wakati wote wanakwenda na wakati  sambamba na mabadiliko ya teknolojia yanayotokea siku hadi siku.
 
Aliwaeleza kuwa TBL Group itaendelea kufanya kazi sambamba na serikali,taasisi zingine na  wananchi kwa ujumla kwenye jamii kuhakikisha  maendeleo endelevu yanapatikana na aliipongeza taasisi ya Swedish Institute kwa kubuni programu ya kuwanoa Vijana wasomi katika mitaala ya uendeshaji biashara kwa mifumo ya kisasa yenye lengo la kuleta ufanisi na kukuza sekta mbalimbali za biashara.
Kwa upande wake Meneja wa mafunzo  hayo kutoka taasisi ya Swedish Institute,Matilda Axelsson,alisema ziara ya mafunzo waliyofanya kiwandani hapo imewawezesha wanafunzi wake kupata maarifa kuhusiana na mifumo bora ya uendeshaji wa viwanda kwa tija.
 
Alisema kuwa taasisi hiyo tangia ianze kutoa mafunzo ya kibiashara na utawala barani Afrika tangia mwaka 2008 imepata mafanikio makubwa ambapo vijana wasomi kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakijiunga kwenye Programu zake za kibiashara kwa ajili ya kunolewa na kuwaanda kuwa waendeshaji wa biashara wazuri “Tutazidi kujipanga kuhakikisha vijana wengi wasomi wanapata fursa za kuhudhuria mafunzo haya na natoa wito kwa waajiri kuwadhamini wafanyakazi wao kupata mafunzo zaidi ili kuleta ufanisi wa kibiashara kupita raslimali watu”.Alisema.

No comments