MAWAZIRI 15 WA NCHI ZA SADC KUKUTANA DAR KESHO
Immaculate Makilika- MAELEZO
Mawaziri
15 wa Nchi Wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika ( SADC), wanatarajia kufanya mazungumzo kesho jijini Dar es
salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya nje
na Ushirikiao wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga alisema kuwa
mawaziri hao wanatarajiwa kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo elimu,
ushiriki wanchi za SADC, ikiwa ni pamoja na kuzungumzia haliinayoendelea nchini Msumbiji.
“Tanzani
ni mwenyeji na wenyekiti wa Mkutano huo, ambapo pia inaongoza Kitengo
Maalumu cha Masuala ya Ulinzi,Usalama pamoja na Siasa, pia kamati ya
siasa na diplomasia inatarajiwa kukutana pia wiki hii” alisema Waziri
Mahiga
Kila mwaka mawaziri hao hukutana mara moja, kwa lengo la kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu nchi wanachama wa umoja huo.Katika
hatua nyingine, Waziri Mahiga alisema kuwa ,Tanzania inashirikiana na
Msumbiji kufanyia kazi suala la watanzania walihamishwa nchini.
“ Hili
ni zuala gumu kidogo tusitoe majibu rahisi, na hivyo Serikali zote
mbili zinaendelea kufanya mazungumzo zaidi juu ya suala hili” alisema
Waziri Mahiga.
No comments