Header Ads

ad

Breaking News

Manchester United, AS Roma zashinda Ligi ya Europa

Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Saint-Etienne, katika mechi ya Kombe la Europa. Mabao ya Man United yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic.
As Roma wakicheza ugenini wameshinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Villarrea, Tottenham Hotspurn wamepoteza mchezo ugenini kwa kuchapwa kwa bao 1-0 na Kaa Gent.
AZ Alkmaar wamelala nyumbani kwa kufunga 4-1 na Lyon, wajerumani wa Borussia Moenchengladbach nao wamepoteza kwa Fiorentina kwa kufungwa bao 1-0.
Athletic Bilbao wameshinda nyumbani kwa 3 - 2 dhidi ya Apoel Nicosia, Celta Vigo wamechapwa na Shakhtar Donetsk kwa bao 1-0. Anderlecht wameshinda 2 - 0 dhidi ya Zenit St. Petersburg.
Paok Thessaloniki wameshindwa kutamba nyumbani kwa kufunga na Schalke kwa 3-0,

Matokeo mengine

Ander Herrera na Daley Blind wakimpongeza Ibrahimovic baada ya kuigfungia bao timu ya United jana kwenye Uwanja wa Old Trafford, Manchester.
Anthony Martial wa Manchester (kulia) akijaribu kufunga bao huku beki wa St Etienne, Kevin Malcuit akiwa makini kumzuia.
Kaka yake Paul Pogba,  Florentin (kushoto) anayeichezea St Etienne na Paul wa Man United  wakiingia uwanjani kabla ya mechi yao kwenye Uwanja wa old Trafford jijini Manchester.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho (kushoto) na Christophe Galtier wa St Etienne ya Ufaransa, wakifuatilia mechi ya Kombe la Europa kwenye Old Trafford jijini Manchester jana.
Paul Pogba akiteta na kaka yake, Florentin (kulia), beki wa St Etienne jana kwenye Uwanja wa old Trafford.
  • Astra Giurgiu 2 - 2 Genk
  • Rostov 4 - 0 Sparta Prague
  • Ludogorets Razgrad 1 - 2 FC Koebenhavn
  • Olympiacos 0 - 0 Osmanlispor FK
  • Hapoel Beer Sheva 1 - 3 Besiktas
  • Legia Warszawa 0 - 0 Ajax

No comments