MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATENDAJI WA MANISPAA YA WILAYA YA ILEMELA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia Watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John
Mongella akihutubia mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa watendaji na
Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe.
Angelina Mabula (kulia) wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais na
Watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Picha ya pamoja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada za
kupambana na dawa za kulevya nchini kama hatua ya kuliokoa na taifa
janga hilo ambalo limesababisha madhara makubwa katika jamii.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri
ya wilaya ya ILEMELA mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa
mapambano dhidi ya dawa za kulevya yatakuwa ni endelevu lengo likiwa
kukomesha kabisa uuzaji,usambazaji na utumiaji wa dawa hizo kama hatua
ya kuokoa kizazi cha sasa na kijacho nchini.
Amesema kamwe serikali ya wamu ya
Tano hatarudi nyuma katika vita dhidi ya dawa za kulenya na ameomba
wananchi waendelee kutoa taarifa za siri kwa vyombo vya dola
zitakazosaidia kuwabaini watu wanajihusisha na biashara hiyo ili waweze
kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kuhusu tatizo la uvuvi haramu,
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa ya
kanda ya Ziwa wakiwemo viongozi wa Mwanza na mikoa mingine nchini
kuanzisha mara moja oparesheni kali ya kupambana na wavuvi haramu katika
Ziwa Victoria ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa samaki
katika Ziwa hilo.
“Viwanda vya samaki kwa sasa
havipati samaki wa kutosha hali ambayo imezorotesha shughuli za
kuchakata samaki hivyo nawaagiza viongozi wote kupambana ipasavyo na
wavuvi haramu na kamwe wasionewe huruma” amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini ni
muhimu yakaenda pamoja na oparesheni ya kukomesha uvuvi haramu katika
Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini.
Amesema wavuvi haramu wamechangia
kwa kiasi kikubwa kupungua kwa samaki katika maziwa mbalimbali nchini
kwa sababu wanatumia nyavu haramu ambazo zinaharibu mazalia ya samaki
hivyo ni lazima hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao ili kukomesha kabisa
tatizo hilo.
Wakati huo huo halmashauri ya
wilaya ya ILEMELA, imetekeleza maagizo 14 yaliyotolewa na Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
aliyoyatoa mwaka jana alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo likiwemo
suala la watumishi wa halmashauri kukaa karibu na maeneo ya ofisi ambapo
mpaka sasa wakuu wa idara 23 wanaishi ndani ya wilaya ya ILEMELA
ikilinganishwa na hapo awali ambapo watumishi hao walikuwa wanakaa nje
ya wilaya hiyo hali ambayo inatajwa ilichangia kuzorotesha utendaji kazi
kwenye halmashauri hiyo.
Kufutia hali hiyo, Makamu wa Rais
Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mlezi wa halmashauri hiyo
amepongeza viongozi wa wilaya hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri
kwa kutekeleza maagiza yake kwa haraka na kwa wakati.
Amesema yeye kama mlezi wa
halmashauri hiyo atahakikisha halmashauri inafanya kazi kwa ubora wa
hali ya juu katika utoaji wa huduma za uhakika kwa wananchi na kuondoa
haraka changamoto mbalimbali zizowakabili wananchi hao ikiwemo
uimarishaji wa miundombinu ya barabara.
No comments